Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 7, 2011

*MATUKIO YA LEO MKOANI SONGEA


Vijana wanadikiwa kuwa ni vibaka katika mitaa ya Manispaa ya Songea wakishikana mashati baada ya mmoja wao kuwadhurumu wenzake mgao wa fedha, baada ya kufaulisha tukio lao la uporaji na kufanikiwa kuuza. Sasa kazi ikwa ni uwiano wa mgao ndiyo chanzo cha kuanza kwa sakata hili la kushikana mashati na kuchapana hadaharani, haikuweza kufahamiaka tukio hilo la uporaji walilitenda katika mtaa gani na kwa mhusika gani. Picha Zote na Muhidin Amri,Songea
Kijana ambaye hakuweza kufahamika jina lake, akiandaa biashara ya ke ya utumbo kama alivyokutwa na mpiga picha Muhidin Amri, mjini Songea jana. Wafanyabiashara hawa wamekuwa na utaratibu wa kufanya biashara kama hii katika maeneo hata ambayo si maalum kwa ajili ya biashara.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Chistine Ishengoma, akiwa ofisini kwake wakati akifanya kikako na watendaji wa ofisi yake na waandishi wa habari hivi karibuni.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya mkoani Ruvuma wakiwa nje ya ukumbi wa Maliasili, wakati wakisubiri kikao cha Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais mazingira, Theresia Luoga, ambapo waandishi hao walisubiri kwa zaidi ya masaaa 4, katika ukumbi wa Maliasili mjini Songea jana.
http://sufianimafoto.blogspot.com/

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...