Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 28, 2011

BURUDANI CLASSIC NDANI YA MZALENDO PUB JUMAPILI


BENDI mpya inayoundwa na wasanii wakali na chipukizi katika anga za muziki wa dansi, Mapacha wa3 wanatarajia kufanya onyesho la pamoja na wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanaotamba katika miondoko hiyo Julai 3 mwaka huu katika ukumbi wa Mzalendo Pub.
Wasanii hao ni pamoja na, Ali Kiba na Elias Barnaba maaarufu Barnabas, ambao watashambulia jukwaa moja na Mapacha wa3.
Mmoja wa wakurugenzi wa mapacha watatu Kharidi Chokoraa maarufu Tora bora amesema Onyesho hilo la pamoja litafanyika Jumapili Julai 3 katika Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama.
Chokoraa amesema lengo la onyesho hilo ni kuwapa ladha tofauti mashabiki wa Mapacha watatu na huenda ikafanyika kila Jumapili ya kwanza ya kila mwezi ili kudhihirisha kwa mashabiki ujio wao wa kutoa burudani hasa katika kiunga cha Mzalendo.
Aidha amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika nawasanii hao watapiga live na bendi hiyo, hivyo mashabiki watarajie kupata burudani ambayo hawajawahi kuipata kutoka kwa wasanii wa ndani.
“unajua Ali Kiba ni msanii mkubwa na ni mkali jukwaani na pia Barnaba ambaye amewahi kuimba na Faly Ipupa, alipokuja nchini na mapacha watatu ndo usiseme ni burudani ya kufa mtu.” Alisema Chokoraa.
Ali kiba amewahi kutamba na nyimbo kama Cinderela, mac Mugn, Karim na sasa anatamba na kibao cha Mapenzi yana run Dunia ambacho kimejizolea umaaarufu mkubwa wakati Barnaba ametamba na vibaon kama Njia panda na mbalamwezi, Nabembelezwa na sasa anaendelea kutamba na kutikisa na kibao chake cha Daima Milele.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...