Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 30, 2011

Isha Mashauzi kumsindikiza Mkubwa Fella katika mpambano wa Nani mkali katika wasanii Kizazi kipya cha Taarab, tarehe 1 July. Equator Grill Temeke!.


Mkubwa FELLA
kiongozi wa kundi la bongo fleva TMK Family yakina Temba na Chegge, ambaye pia ni msanii chipukizi ktk Taarabu atachuana na wasanii wengine watatu chipukizi ktk miondoko hio ya muziki wa Taarabu ktk kumtafuta Mkali nani kati yao Ijumaa hii pale EQUATOR GRILL, Mtoni kwa Aziz Ally

Show hio ya aina yake itaanza mishale ya saa 2 usiku huku ikiongozwa na Kings Modern Taarab wanaotamba na nyimbo kibao kwasasa ikiwemo "Kijoka" na kusindikizwa na ISHA MASHAUZI mkali wa "Mama nipe Radhi" na zingine nyingi.

Wasanii wa kizazi kipya cha Taarab watakaopanda jukwaani kuoneshana nani mkali ni wale wanaotamba sana ktk medani hizo ambao ni Mkubwa Said Fella na nyimbo yake ya "Simuachi"aliyomshirikisha Isha, Athumani Ally "Nyongo mkalia ini", Omary Ally "Simuachi mpenzi wangu" na Kepteni Temba "Nimeiteka himaya".


Akimalizia kunihabarisha mratibu wa onyesho hilo la mpambano alisema kiingilio kitakuwa ni Tshs. 5000/= na wapenzi na mashabiki wote wa burudani kutoa maamuzi NANI MKALI KATI YAO!!!!!!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...