Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 8, 2011

MWALIMU, MCHUNGAJI WA KKKT ATUPWA JELA MVUA 6 KWA KUOMBA RUSHWA YA MAPENZI


MAHAKAMA ya Hakimu mkazi mkoa wa Iringa, imemhukumu kwenda jela miaka sita, mwalimu wa shule ya Sekondari ya Pomerini wilaya ya Kilolo mkoani iringa, Michael Ngilangwa, Mchungaji wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Njombe baada ya kupatikana na kosa la kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake. Pichani ni mchungaji huyo akiwa chini ya ulinzi wakati akipelekwa kupanda karandinga kuelekea jela. Francis Godwin, Iringa anaripoti.

Hukumi hiyo imetolewa na Hakimu Martha
Mpaze jana baada ya mwalimu huyo kupatikana na hatia katika mashtaka mawili yaliyokuwa yakimkabili katika kesi iliyofunguliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (Takukuru) mkoa wa Iringa.

Alisema:- "Mahakama imerizishwa na ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo
vilivyowasilishwa mahakani hapo hivyo ili iwefundisho kwa wengine mahakama inatoa adhabu kali dhidi ya mshitakiwa kwa kumhukumu kutumikia adhabu ya miaka sita jela" alisema Hakimu.
Aidha katika kosa la kwanza mwalimu huyo anadaiwa kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake huyo jina (limehifadhiwa) ili kumsaidia masomo ambapo adhabu yake ni kulipa faini ya shilingi laki tano ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, na kosa la pili ni kutaka kumbaka mwanafunzi huyo ambapo mahakama hiyo inamhukumu kwenda jela miaka mitano.
http://sufianimafoto.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...