Street University inatafuta wajasiriamali 200 tu ambao wanapenda kukuza biashara zao mara mbili au zaidi ya zilivyo sasa kwa msaada wa karibu wa waalimu na wataalamu wa ujasiriamali, wahadhiri wa Street University, Eric Shigongo na James Mwang’amba.
Ukiwa mmoja wa wanafunzi hao utashikwa mkono kwa mkono na makocha hao wa biashara ili uweze kufanikisha malengo yako.
Programu hii itaanza tarehe 23 Machi mwaka huu, na nafasi zitatolewa kwa watakaowahi kujiandikisha na watakaostahili.
Washiriki watasajiliwa kama wanachama wa Street University bure na kupewa vitabu, DVD na CD za Shigongo na Mwang’amba bure. Pia watasaidiwa kila mwezi kwa miezi sita mfululizo ijayo kuleta mabadiliko kwenye biashara zao. Kwa maelezo ya ziada na jinsi ya kujiunga, tembelea tovuti yetu hii au piga simu 0222773356 au fika ofisi za Global Publishers Ltd (GPL) zilizopo Mwenge-Bamaga kwa ajili ya kipeperushi na fomu za kujiunga.
PROGRAMU ITAKUWA NA YAFUATAYO:
- Siku tatu za mafunzo ya umakini mkubwa kuhusu masuala yote muhimu ya kuanzisha na kuendeleza miradi mbalimbali ili iweze kuleta faida, ikiwa ni pamoja na misaada ya fedha, utafiti wa masoko, mauzo, kuwaelewa wateja husika, na masuala ya utawala na uongozi. Siku hizo ni tarehe: 23 Ijumaa, 24 Jumamosi na 25 Jumapili mchana.
- Misaada mbalimbali kila mwezi kwa njia ya simu au barua pepe.
- Utoaji wa bure wa vitu mbalimbali vinavyohusiana na ujasiriamali ambavyo ni pamoja na vitabu, DVD na CD za hotuba za James Eric Shigongo juu ya mbinu muafaka katika kufanikisha ujasiriamali.
- Watu wote watakaohudhuria mafunzo hayo watapewa vitu hivyo bure katika mwezi wa kwanza.
- Katika kila somo patatolewa vitu na taarifa mbalimbali zinazohusika kwa ajili ya ufuatiliaji wa mafunzo.
- Wakati wa mafunzo washiriki watapewa chai wakati wa mapumziko na chakula cha mchana kwa siku zote mbili ambapo siku ya mwisho patatolewa vinywaji baridi.
- Gharama kwa kila mshiriki ni 250,000/.
JINSI YA KUJISAJILI:
1. Tembelea mtandao wa http://streetuniversity.co/ ili uelewe mambo mengi zaidi.
2. ‘Download’ fomu husika na uijaze.
3. Lipia gharama husika kupitia akaunti ya benki ya CRDB 01J2021254000 au
M-PESA 0767 797779.
4. Tupigie simu ili kuthibitisha kukubaliwa kwako.
MASOMO YATAKAYOTOLEWA SIKU HIZO TATU:
- Jinsi ya kuwa na ubunifu au uvumbuzi wa mbinu za kuendeleza biashara.
- Jinsi ya kujenga mazingira mazuri ya kuvutia wateja wako.
- Kupanua zaidi masoko ya biashara yako.
- Uwezo wa kuendeleza mauzo yako vizuri katika mazingira ya uchumi mbaya.
- Kuhakikisha biashara yako inakuwa na hadhi ya juu zaidi.
- Maarifa yatakayohakikisha unalitawala soko la biashara yako.
FOMU ZA KUJIUNGA ZINAPATIKANA KATIKA LINK HII:
http://streetuniversity.co/wp-
No comments:
Post a Comment