Mchezaji wa timu ya Simba Felix Mumba Sunzu akimkabidhi jezi yake mgeni rasmi Naibu Waziri wa TAMISEMI Bw. Kassim Majaliwa aliyopewa katika hafla ya uzinduzi wa Televisheni ya klabu ya Simba ambayo itaanza kwa kurusha vipindi vya mambo mbalimbali yanayohusu klabu hiyo na baadae kuanza kurusha vipindi vyake masaa 24, hafla hiyo imefanyika jana usiku Quality Center jijini Dar es salaam. Katika picha kushoto ni shabiki mkubwa wa timu hiyo Profesa Juma Kapuya na kutoka kulia ni Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Geofrey Nyange Kaburu na Mwenyekiti wa klabu hiyo Mh Ismail Aden Rage.
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba Zamoyoni Mogella akizungumza katika uzinduzi huo na kuwaasa wachezaji wa timu ya Simba kuonyesha uwezo wao wote hasa katika mchezo wa kesho kati ya Simba na Kiyovu ya Rwanda , kulia ni msemaji wa klabu ya Simba Ezekiel Kwamwanga.
Mgeni rasmi Naibu Waziri TAMISEMI Kassim Majaliwa akimisha keki Mwenyekiti wa klabu ya Simba Mh Aden Rage wakati wa hafla hiyo, kutoka kushoto ni Makamu wa pili wa TFF Bw. Ramadhan Nassib, Profesa Juma Kapuya na kulia ni Mzee Kinesi.
Mgeni rasmi Naibu Waziri TAMISEMI Kassim Majaliwa akikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa televisheni hiyo, kutoka kushoto ni Makamu wa pili wa TFF Bw. Ramadhan Nassib,Profesa Juma Kapuya, kulia ni Mzee Kinesi na Meneja wa Kinywaji cha Kilimanjaro George Kavishe.
Mgeni rasmi Naibu Waziri TAMISEMI Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kwenye kompyuta tayari kwa kuwasha kipindi cha Televisheni kinachoonyesha matukio mbalimbali ya klabu ya Simba, Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu, Shakibi wa Simba Mh. Profesa Juma Kapuya na kutoka kushoto ni Ezekiel Kamwanga Msemaji wa klabu ya Simba na Ismail Aden Rage Mwenyekiti wa Simba.
Shabiki mkubwa wa Yanga Motisha naye alihudhuria katika sherehe hiyo hapa akitambulishwa huku Kocha wa makipa wa Simba Bw. Kisaka akimuwekea Jezi ya Simba ama kwa huu ndiyo utani jamani.
mungu aisaidie simba na awangamize maadui wa simba.
ReplyDeleteTulicoanzisha kisirudi nyuma kiwe ni mbele kwa mbele.
Heko na hongera kwa wnasimba wote
mungu aisaidie simba na awangamize maadui wa simba.
ReplyDeleteTulicoanzisha kisirudi nyuma kiwe ni mbele kwa mbele.
Heko na hongera kwa wnasimba wote