
Shukrani za pekee ziwaendee Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Aga Khan ambao walikuwa wakipigania ili kuokoa maisha ya mpendwa marehemu Mama yetu bila kuchoka hadi dakika ya mwisho neno la Mungu lilipotimia.
Shukrani pia ziwaendee Familia yote ya Marehemu Dr. Luhangano Joseph Badi ikiongozwa na Dada yetu Mkubwa Mama Blandina Nyoni, shemeji zetu kwa jitihada walizozifanya za kujaribu kuokoa maisha ya Mama yetu.
Pia nawashukuru Wanahabari, Bloggers na wadau wote ambao kwa namna moja ama nyingine walijumuika nami katika kunifariji na kunitia moyo katika kipindi hiki kigumu, ama kwa njia ya simu, E-mails, ana kwa ana.
Si rahisi kumtaja mtu mmoja mmoja ila shukrani pia ziwaendee Mama Mdogo Eliza, Binamu zetu pamoja ndugu jamaa na marafiki.
Sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mungu abariki kila jambo mnalolifanya hapa duniani na hakika mmejiwekea thawabu nyingi kwake. Kwa kuwa kila nafsi itaonja mauti, basi hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutimiza ahadi yake na tuseme: Yeye (Mama Esther Nyimbo Badi) ni wa Mwenyezimungu na kwake Mungu sote tutarejea!
Mungu ampumzishe Mama Esther Nyimbo Badi Mahala Pema Peponi – Amen!
No comments:
Post a Comment