Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, October 21, 2013

CANNAVARO, AGGREY MORRIS WATEMWA ZANZIBAR, KUKOSA CHALENJI MWAKA HUU
KIKOSI cha wachezaji 30 cha timu ya taifa ya Zanzibar kimetangazwa na kocha mkuu wa timu hiyo Salum Bahusi bila ya jina la nahodha wa Yanga, Nadir Haroub Cannavaro na Aggrey Morris wa Azam FC.
Kwa mujibu wa habari kutoka Zanzibar, kikosi hicho ambacho kinatarajiwa kushiriki Kombe la Chalenji kuanzia Novemba 27 mwaka huu jijini Nairobi Kenya, Kocha wa Zanzibar Heroes, Bausi amesema kikosi hicho kitaingia kambini Oktoba 27 mwaka huu na keshokutwa jumatano wachezaji wote walioitwa kikosini watafanyiwa vipimo.
Katika kikosi kilichotajwa leo, MAKIPA ni Mwadini Ali (Azam), Abdallah Rashidi (Ruvu Shooting), Ali Suleiman (KMKM).
MABEKI ni Mohamed Azan (Polisi), Waziri Salum (Azam), Shafi Hassan (Malindi), Mohamed Faki (Zimamoto), Salum Haji (Miembeni), Said Yussuf (Mtende), Mohamed Othman (Jamhuri), Mussa Said (Chwaka Stars), Nassor Masoud ‘Chollo’ kutoka Simba.
VIUNGO ni Abdulhalim Humud (Simba), Sabri Ali (JKT Oljoro), Adeyum Saleh (Simba), Isihaka Othman (JKU), Ali Kani (JKT Oljoro), Hamad Mshamata (Chuoni), Suleiman Hamad (Miembeni), Awadh Juma na Masoud Ali wote wa Mtibwa Sugar.
WASHAMBULIAJI ni Seif Karihe (Azam), Suleiman Kasim Solembe (Coastal Union), Khamis Mcha (Azam), Amour Omary (Miembeni), Amir Hamad (JKT Oljoro), Jaku Joma (Mafunzo), Faki Nahoda (Kimbunga), Hassan Seif (Mtibwa Sugar), Juma Ali Yussuf wa New Generation.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...