Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 31, 2013

ROMA ATANBULISHA VIDEO YA '2030' KESHO


Na Elizabeth John


ILE video ya wimbo unaojulikana kama ‘2030’ iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki wa hip hop nchini, ulioimbwa na mkali wa muziki huo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ inatarajiwa kuzinduliwa Novemba Mosi.
Kwa mujibu wa msanii huyo kupitia ukurasa wake wa Facebook, alisema mashabiki wa muziki huo wakae mkao wa kula kuipokea video ya wimbo huo ambao upo sokoni tangu Januari mwaka huu.
“Mashabiki wangu wameisubiri kazi hii kwa siku nyingi sana naomba wakae mkao wa kula kuipokea kazi hii ambayo naamini itakuja kuliiteka soko la muziki huo kutokana na maudhui ya wimbo huo,” alisema.
Alisema anatarajia kuanza kuisambaza katika vituo mbalimbali vya televisheni, Ijumaa ya wiki hii hivyo mashabiki wake wasubili kuona kilichozungumzwa katika wimbo huo.

Roma ni kati ya wasanii wa hip hop Tanzania ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo kutokana na mashairi ya nyimbo zake kusimama na kuwa na ujumbe mzito katika jamii inayomzunguka.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...