Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 31, 2013

TIMBULO AIPIKA 'BADO INATAMBA'
Na Elizabeth John


NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ally Timbulo ‘Timbulo’, amewaomba mashabiki wa muziki wa kizazi kipya nchini, wajiandae kupokea kibao chake kipya kinachokuja kwa jina la ‘Bado Inatamba’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Timbulo alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho, ambacho anaamini kitakuwa gumzo mtaani kutokana na ujumbe uliopo.

Alisema wimbo huo utakuwa ni changamoto kwa wasanii wenzake, kutokana na baadhi ya ujumbe uliopo ndani ya wimbo huo unaowaonya wasanii kuwa na nyimbo zenye manufaa kwa jamii.

“Kiukweli wasanii wengi wa bongo fleva, tumekuwa tukipeleka mawazo yetu kwenye mapenzi pekee, mimi nimeona kuondoka kwenye mapenzi na kufanya kazi ambazo zinaelimisha jamii kwa kiasi kikubwa,” alisema Timbulo.

Licha ya kutaka kutoka na kibao hicho, Timbulo alishawahi kutamba na vibao vyake kama, ‘Samson na Delila’, ‘Timbulo wa leo’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...