Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 25, 2013

MWANAMUZIKI MOHOMBI AWASILI JIJINI DAR , TAYARI KUTUMBUIZA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA KESHO JUMAMOSI LEADERS CLUB  Msanii wa kimataifa Mohombi Nzasi Moupondo baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere kwa ajili ya shoo kali ya Serengeti Fiesta  itakayofanyika kesho katika viwanja vya Leaders Club. Mbele yake ni Fauzia mratibu wa shughuli za Serengeti Fiesta kutoka PrimeTime Promotions.

 Msanii wa kimataifa Mohombi Nzasi Moupondo  (kulia) akifanya interview na wanahabari baada ya kutoka nje ya uwanja wa ndege kwa ajili  ya kufanya shoo kali ya Serengeti Fiesta inayotarajiwa kufanyika kesho  katika viwanja vya leaders club. Tamasha hilo limedhaminiwa na kampuni ya  bia ya Serengeti kupitia bia ya Serengeti Laga.

 Mohombi (kulia) akisindikizwa kutoka nje ya uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere  baada ya kushuka na ndege ya Turkish Air lines na Afisa wa ndege hiyo Ebubekir Ekici ambaye pia alifurahia ujio wake Tanzania.

Msanii wa kimataifa anaetamba na kibao chake kikali cha “Kiss Me” akiwa amepozi na mtangazaji wa Clouds Tv baada ya kupokelewa jana katika  uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...