Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, October 21, 2013

Redd's Uni-Fashion Bash ndani ya jiji la Mwanza ni raha tupu Meneja wa Mauzo ya Rejareja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda la Ziwa,Andrew Mbwambo (kulia) akikabidhi kitita cha Sh. Laki 7 kwa Mshindi wa Kwanza wa Ubunifu wa Mitindo kwenye Redd's Uni-Fashion Bash,Dotto Elias (kutoka Chuo cha Biashara cha CBE jijini Mwanza) baada ya kuwagaragaza wenzake,katika Tamasha hilo lililofanyika kwenye Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini,Mwanza.
 Meneja wa Mauzo ya Rejareja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda la Ziwa,Andrew Mbwambo (kulia) akikabidhi kitita cha Sh. Laki 5 kwa Mshindi wa Kwanza wa Mitindo kwenye Redd's Uni-Fashion Bash,Fahad Rajab (kutoka Chuo cha Mt. Augustine ya jijini Mwanza) baada ya kuwagaragaza wenzake,katika Tamasha lililofanyika kwenye Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini,Mwanza.
 Mkali Muziki wa Kufoka hapa nchini,Fareed Kubanda a.k.a Fid Q akitoa burudani kwa wakazi lukuki wa Jiji la Mwanza waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini,Mwanza kushuhudia Tamasha la Redd's Uni - Fashion Bash.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...