Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 24, 2013

MWANAMKE MAKETE MBARONI KWA KUMMWAGIA MWENZIE MAJI MOTO NA KUMJERUHIJeshi la polisi wilayani Makete mkoa wa Njombe linamshikilia Bi Rose Skwea Tweve mkazi wa kijiji cha Isapulano kwa tuhuma za kummwagia maji ya moto mke mwenzake Estina Kristian Sanga [23] pamoja na mtoto wake mdogo ambao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Makete kwa matibabu zaidi.

akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mrakibu wa polisi ambaye pia ni afisa upelelezi (OCCID) wilaya ya makete Gosbert Komba amesema matukio ya kujichukulia sheria mkononi yamekuwa yakijirudia mara kwa mara wilayani hapo huku akiwataka wananchi kufuata sheria na taratibu za nchi.

kwa upende wake Bi Estina Sanga Ambaye amejeruhiwa na mke mwezake huyo amesema kuwa tukio hilo lilimpata majira ya saa mbili usiku alipokuwa anakwenda kumjulia hali mume ambae ni mgonjwa nyumbani kwa Bi Rose ambaye ni Bi mkubwa. 

Naye mtuhumiwa wa tukio hilo Bi Rose Tweve amesema alifikia hatua hiyo baada ya kurushiana maneno na mke mweziye huyo na kuchukizwa kwa kitendo cha kwenda kumuona mume wao huku akiwa amelewa ndipo akachua sheria mkononi kwa kumwangia maji ya moto ka njia ya kumuonya. 

akizungumzia tukio hilo Bwana Itiso Chaula (32) ambaye ni mume wa wanawake hao mkazi wa kijiji cha Isapulano amesema ameshangazwa na tukio ambalo Bi mkubwa amelifanya kwa Bi mdogo na kulaani kitendo hicho.
Occid Komba amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi huku upelelezi ukiendelea, lakini amesema kwa taarifa alizonazo majeruhi anaendelea na matibabu baada ya kujeruhiwa na maji moto usoni na maeneo ya kifuani
NA EDWIN MOSHI, GLOBU YA JAMII MAKETE

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...