Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 25, 2013

KONYAGI YASHINDA UBORA WA BIDHAA, YAPAA KWENDA HISPANIA KUCHEKI KABUMBUMkurugenzi Mkuu wa TDL akiwa na Mabosi wa SABMILLER AFRICA.wakiwa wameshikilia tuzo hiyo ya  MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR (F 13)


PICHA NDOGO CHINI NI BAADHI YA WAFANYAKAZI TDL WALIO TEULIWA KWENDA KUTIZAMA KABUMBU UGHAIBUNI
                                                            MWEISIGA MZEE WA JIJI
                                                 CHIBEHE MZEE WA TANZANIA
                                                    BI, KHADIJA MKUU WA MSAFARA
                                       HUYU NDIO MREMA MZEE WA MWANZA

 
KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Ltd (KONYAGI) imeshinda tuzo ya utendaji bora wa bidhaa (SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13), ni miongoni mwa Kampuni tanzu za Sabmiller ya Afrika Kusini.

Akiongea na waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi ya  Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa, aliyepambana mpaka kupatikana kwa ushindi huo. amesema kuwa wanajivunia kuwa washindi miongoni mwa makampuni mengi yaliyo chini ya Sabmiller.

“Ushindi huu ni ishara kubwa ya mafanikio KONYAGI na sisi hatutarudi nyuma hii ni chachu katika kutufanya tuendelee kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango vya hali ya juu kwa bei nafuu na kuzishinda kampuni zingine” alisema Mgwassa.

Amesema kuwa ushindani ulikuwa mkubwa sana mana kila Kampuni miongoni mwetu inajitahidi kuzalisha bidhaa kwa kiwango cha hali ya juu na sisi kushinda ni ishara kuwa bidhaa zetu zinakubalika kila mahali hapa Africa hata nje ya Africa.

                                                            ZAWADI YA KWENDA

Licha ya kupewa tuzo ya ubora, pia TDL imepewa nafasi kwa Wafanyakazi wake watano kwenda kuangalia mpambano mkubwa la ligi kuu  ya Hispania (LA LIGA) kati ya Barcelona na Real Madrid.
Mgwassa aliwataja wafanyakazi wanaokwenda Hispania kuangalia mechi hiyo kuwa ni Joseph Chibehe, Khadja Madawili, Bavon Ndumbati, Michael Mrema na Mwesige Mchuruza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...