Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 17, 2013

SASA KALAMA NYILAWILA KUMVAA SADO PHILEMON NOVEMBA 3 CCM MWIJUMAKALAMA NYILAWILA
MPAMBANO wa masumbwi uliokuwa uwakutanishe kati ya Bondia Kalama Nyilawila na Sado Philemon  uliokuwa uchezwe Oktoba 20 jumapili katika uwanja wa CCM Mwijuma Mwananyamala umeailishwa kutokana na kupisha mpambano wa watani wa jadi simba na yanga utakaofanyika katika uwanja wa taifa

akiongea mratibu wa mpambano huo Ibrahimu Kamwe 'amesema mpambano huo umeailishwa kwa muda kupisha mchezo wa simba na yanga kwa kuwa mashabiki wa mpira ndio hawo hawo mashabiki wa mchezo wa masumbwi hivyo kwa sasa mpambano uho utafanyika Novemba 3 katika ukumbi uho huo mpambano huo uliokuwa uwakutanishe mabondia mbalimbali wakongwe na chipkizi sasa utachezwa siku hiyo alitaja mapambano ambayo yatakuwepo kuwa '

Mwaite Juma na Shadrack ignas , nae bingwa wa zamani wa bantam  Ajibu salum atapimana ubavu na Martin Richard,huku  mbena Rajab akizipiga na Godwin Mawe, Ibrahim class 'King Class Mawe ' atazichapa na Rashid Ali, Hassan kiwale (Moro best) na Harman Richrd, Kasim chuma na Shaban Manjoly, mdogo wake francis miyeyusho  Yona miyeyusho  atacheza na julias Thomas, Abdalla ruwanje na Bakari zoro, na kutakuwepo na pambano la kitaa kwa mbabe wa mwananyamala sokoni  joseph stanslaus(amita au jose mawe) na mbabe wa manzese sokoni  shaban seif(body kitongoji) pambano lililojaa vituko na mbwembwe kwa mabondia hawa, nae  yasin omari  atazichapa na Innocent Gabriel pamoja na mapambano  mengine kadhaa ya vijana wadogo wenye vipaji  vya mchezo wa ngumi. Mapambano haya yote yameandaliwa na Ibrahim kamwe wa bigright promotion  kwa kusindikiza pambano la ISSA OMAR(peche boy) atakaezipiga  na  ATHONY MATHIAS katika pambano la round nane na SADO PHILEMON    atakaezipiga na KARAMA NYILAWILA katika uzito wa middle kutafuta mshindi  wa atakaezipiga na Thomas mashali katika pambano la ubingwa.kwa ufupi mabondia wote wapo katika hali nzuri na wametakiwa kuendelea na mazoezi kwa ajili ya mpambano utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika ukumbi wa ccm mwinjuma mwananyamala A

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...