Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 31, 2012

Afande Sele anaukaribisha mwaka mpyaNa Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ anajipanga kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Soma Ule’ ambayo itakua ngoma ya kuukaribisha mwaka 2013.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Afande Sele alisema wimbo huo utakua ujumbe wa kufungia mwaka na kuukaribisha mwaka mpya na kwamba yupo katika hatua za mwisho za uaandaaji wa kibao hicho.

“Audio nishamaliza saivi nafanya video, unajua redio saivi hazina soko sana watu wengi wanapenda kuangalia na sio kusikiliza, hivyo namalizia kurekodi video baada ya hapo ntaipelela sokoni, kikubwa ni sapoti kutoka kwa mashabiki,” alisema Afande Sele.

Mbali na hilo, Afande Sele alisema kwasasa wanaendelea na mchakato wa kusaidia jamii kwa kutoa fedha pamoja na vifaa vya hospitalini kama shukrani kwa wadau wa kazi zao, ambapo unaongozwa na mkali wa muziki huo, Joseph Haule ‘Professa Jay’.

“Professa kaanzisha mchakato huo, ambao unajulikana kama ‘Nishike mkono’ na hivi karibuni tumesaidia vifaa katika hospitali ya watoto  ya Tumbi iliyopo kibaha, hivyo tunaomba sapoti kwa wadau wa muziki na mashabiki wa kazi zetu,” alisema Afande Sele.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...