Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 26, 2012

shabani kilumbelumbe vs imanuel naidjalabondia chipukizi mtanzania shabani kilumbelumbe tarehe 13-11-2012 anatarajiwa kupanda ulingoni jijini windhock- namibia kuzipiga na bondia immanuel naidjala -the prince- wa namibia katika pambano la raundi 12 kugombea ubingwa wa
WBO-AFRICA .

Pambano hilo ni la uzito wa bantam-kgs 53.5 na litafanyika katika ukumbi wa windhock country club resort.


promota wa pambano hili ni NESTOR TOBIAS wa NESTOR SUNSHINE BOXING AYA NCHINI NAMIBIA.


TPBO tayari imeshapata barua ya mwaliko kutoka chama cha ngumi na mieleka cha namibia na mktaba wa bondia pia umeletwa kwa TPBOkupitia wakala wa pambano hili ndg julius odhiambo wa kenya .tayari meneja wa bondia huyu kilumbelumbe mwalimu HATIBU ameshapewa taarifa kuhusu bondia wake kukabiliwa na pambano hili chini namibia.
TPBO INAMTAKA MENEJA WAAKE KUMUANDAA BONDIA WAKE VYEMA KWA AJILI YA PAMBANO HILO ILI AKAFANYE VYEMA.


TPBO IMECHOSHWA SANA NA MAJIGAMBO YA MABONDIA WA KITANZANIA AMBAO HUPATA MIALIKO YA KWENDA KUPAMBANA NJE YA TANZANIA


LAKINI KILA WAKIENDA HUKO HUDUNDWA NA WARUDIPO HUWAKIMBIA WAANDISHI WA HABARI ILI WASIHOJIWE JUU YA KUDUNDWA KWAO.


NAWATAKA MABONDIA WA KULIPWA WAACHE KUONGEA SANA NA BADALA YAKE WAJIANDAE VYEMA KWA MAPAMBANO YAO


BY -YASSIN ABDALLAH -USATAADH


RAIS-TPBO

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...