Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 31, 2012

REDDS MISS TANZANIA YATANGAZA VIINGILIO NA WASANII 31 Oktoba 2012 .Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim Lundenga kulia akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanza kuuzwa kwa tiketi za shindano la Taifa la Redds Miss Tz kushoto kwake ni katibu mkuu wa kamati ya Miss Tz Bosco majaliwa

Fainali za shindano la Redds Miss Tanzania 2012 zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel,  Ubungo Plaza jijini D’salaam
Akizungumza na waanmdishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim Lundenga alisema maandalizi yote yamekamilika na kila kitu kipo tayari na leo tupo hapa kuwatangazia watanzania na washika dau wote wa tasnia ya Urembo kuwa tiketi kwaajili ya shindano letu la mwaka huu zipo tayari na zipo kwa idadi maalum na leo hii zinaanza kuuzwa katika vituo tulivyovipendekeza kulingana na maoni ya wadau
Kutokana na ukubwa wa shindano kwa mwaka huu wale wote watakaofanikiwa kuingia ukumbini watakaa katika viti maalum vilivyowekwa katika hadhi ya kimataifa na kila tiketi itagarimu kiasi cha shilingi laki moja (100,000) za kitanzania.
Katika kufanikisha shindano hili kutakuwa na vitu tofauti na miaka ya nyuma na tutarajie kuona shindano lenye ushindani mkubwa hasa kwa kuzingatia kuwa sehemu kubwa ya warembo wetu ni wasomi walio katika ngazi ya elimu ya juu nchini
Vituo vinavyoanza kuuza tiketi hii leo ni. Stears samora
Regency park Hotel,Rose garden Mikocheni,Share illusion-Mlimani City,Giraffe Hotel,Ubungo Plaza na ofisi za Lino.
Nitoe rai kwa wapenzi wote waweze kupata tiketi mapema ili kuepuka usumbufu kwa sababu ya kikomo cha tiketi kilichopo kama tulivyotangaza awali
Kwa upande wa burudani kutakuwa na burudani nyingi sana na zitaongozwa nawasanii nguli hapa nchini kama
1)   Diamond Platnum
2)   Winfrida Josephat’Rachel’
3)   Wanne star ngoma troupe
Katika shindano hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo yanayojulikana kama [Fast Tract] Tayari washiriki 5 wameshajipatia tiketi ya kuingia katika kundi la Warembo 15 Bora.     [Top 15 Finalist]
Washiriki hao ni
Lucy Stephano – Miss Photogenic
Magdalena Roy – Top Model
Mary Chizi – Top Sport Woman
Babylove Kalalaa – Miss Talent
City sports lounge-iliyopo posta mpya mkabala na mnara wa askari.
Happiness Daniel – Miss Personality
Mwisho napenda kutoa shukrani zangu kwa wadhamini wetu ambao ni TBL kupitia kinywaji chao cha Redds Original,Star Tv na Giraffe Hotel
HASHIM LUNDENGA.
MKURUGENZI

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...