Bondia kutoka nchini Namibia Gottlieb Ndokosho ambaye alimsambaratisha Mtanzania Rajabu Maoja katika raundi ya kwanza ya mpambano wao wa kugombea mkanda wa IBF Afrika katika uzito wa unyoya, atapanda tena ulingoni jijini Windhoek, Namibia kutetea mkanda wake kati ya mabondia watatu ambao walipendekezwa na IBF.

Pambano hilo litakalofanyika katika jiji la Windhoek nchini Namibia utatoa upinzani mkali sana kati ya mabondia hao wanaochipukia vyema.

Kati ya majina matatu yaliyopendekezwa na IBF limo jina moja na Mtanzania Fredy Sayuni ambaye anaishi jijini Dar-Es-Salaam. Wengine ni Patric Okine kutoka Ghana na David Kiilu kutoka nchini Kenya.

Wakati huo huo IBF imetoa kibali kwa bondia Helene Joseph wa Nigeria kutoka barani Afrika kupigania ubingwa wake wa dunia. Mpambano huo utawakutanisha Helen Joseph kutoka nchi ya Nigeria akikutana na bondia Dahianna Santana kutoka Dominican Republic huko Latin America ambaye ndiye bingwa wa dunia wa IBF katika uzito wa unyoya (featherweight) kwa upande wa wanawake.
Helen Joseph
Mpambano huo utafanyika Decemba 1 katika jiji la San Domingo na litasimamiwa na Rais wa IBF kutoka bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba za Uarabu na Uajemi, Mtanzania Onesmo Ngowi.
Picha ya (kulia) Bondia Santana kulia, akiwa ulingoni.
Bondia Helen Joseph ameshapigana mapambano 13 na amepoteza moja wakati mpinzani wake Dahianna Santana amepigana mara 37 na kupoteza mara 6.

*Uongozi*
*IBF Africa, Masharikim ya Kati, Ghuba za Uarabu na Uajemi*
*Dar-Es-Salaam*