Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 31, 2012

DOKEZO LA AMIR MHANDO KUTOKA TASWA


Naomba kuwajulisha kuwa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) na Muungano wa Kamati za Olimpiki za Afrika (ANOCA) kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) wameandaa mafunzo kwa waandishi wa habari wanawake wa Afrika itakayofanyika Desemba 10 na 11 mwaka huu Nairobi, Kenya.

Kutokana na hali hiyo Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimepewa nafasi ya waandishi wa habari wanawake watatu washiriki kwenye mafunzo hayo na imepokea barua hiyo leo na inatakiwa hadi Ijumaa wiki hii iwe tayari majina hayo yametumwa pamoja na wasifu wa wahusika walioteuliwa.

Kwa msingi huo kwa kutumia njia hii ya uwazi zaidi, naomba waandishi wanawake wenye nia na muda wa kushiriki mafunzo hayo wawasilishe CV zao kabla ya Ijumaa (Novemba 2, 2012) saa sita mchana ofisini kwa Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto (Hifadhi House ghorofa ya 9 zilipo ofisi za JamboLeo, Posta)  au kwangu mimi ofisi za Daily News Tazara, Dar es Salaam.

Masharti ya mafunzo ni kuwa yataendeshwa kwa lugha ya Kingereza na Kifaransa, lakini pia watakaoshiriki wawe tayari kuja kutoa elimu watakayaoipata huko kwa wenzao pindi watakaporudi nchini.

Suala la CV ni la umuhimu kupita maelezo, kwani baada ya hapo mchana siku hiyo TASWA itateua majina matatu na kuyatuma TOC kwa taratibu nyingine.

Watakaoteuliwa watalipiwa nauli ya kwenda Nairobi na kurudi Dar pamoja na malazi na chakula kwa siku zote watakazokuwa huko.Tuchangamkie nafasi, kumbuka ni kwa wanawake tu.

Nawasilisha kwa utekelezaji.(Kama hujaelewa tuwasiliane 0713415346)
Katibu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...