Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 18, 2012

LUKAZA EXCLUSSIVE: LUKAZA BLOG YATIMIZA MIAKA 2 TOKEA KUANZISHWA KWAKE.


LEO NI SIKU AMBAYO LUKAZA BLOG ILIANZA KAZI RASMI KWA MARA YA KWANZA KATIKA TASNIA HII YA HABARI KWA KUPITIA MTANDAO WA INTERNET.
NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII MIMI KAMA MMILIKI WA JUKWAA HILI LA HABARI LA LUKAZA BLOG KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KABISA KATIKA SIKU HII AMBAYO NI MUHIMU SANA KWANGU KWA KUSHEREHEKEA LIBENEKE HILI KUFIKISHA MIAKA 2 TOKEA KUZALIWA KWAKE.
 VILEVILE NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII KUWASHUKURU WASOMAJI WA MTANDAO WA LUKAZA BLOG KWA MAANA BILA WAO BLOG HII PENDWA KABISA YA LUKAZA BLOG ISINGEFIKA HAPA ILIPOFIKA LAKINI PIA NACHUKUA NAFASI HII KUWASHUKURU BLOGGERS WENZANGU WOTE AMBAO TUMEKUWA KAMA NDUGU WA BABA MMOJA AMBAPO TUMEWEZA KUSHIRIKIANA KATIKA HALI IWE RAHA AU MATATIZO NA TUMEWEZA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO, AMANI NA UPENDO NAOMBA UMOJA HUU UENDELEE NA KUFIKISHA TASNIA HII SEHEMU YA MBALI ZAIDI YA HAPA TULIPOFIKIA.

KIUKWELI LUKAZA BLOG IMEKUA KWA KIASI KIKUBWA SANA UKILINGANISHA NA WAKATI INAANZA NAJIFUNZIA MAFANIKIO HAYO MADOGO AMBAYO NIMEFIKIA LEO HII LAKINI SAFARI BADO NI NDEFU KATIKA KUFIKIA MALENGO.

LEO TAREHE 18 MWEZI WA 10 2012 LUKAZA BLOG INATIMIZA MIAKA 2 TOKEA KUANZISHWA KWAKE NA MPAKA SASA IMEWEZA KUWAFIKIA WATU WENGI NDANI NA NJE YA NCHI. TUNAPENDA KUWAHAKIKISHIA WASOMAJI WETU KUWA TUTAJITAHIDI SANA KATIKA KUHAKIKISHA HUDUMA ZETU ZINAKUWA BORA NA TUTAJITAHIDI SANA KUHAKIKISHA LUKAZA BLOG INAKUWA NA NAFASI KATIKA MAISHA YAKO AMBAPO UTAKUWA UKIPATA KILA KITU CHINI YA MWAMVULI MMOJA.

TUNASHUKURU MPAKA SASA LUKAZA BLOG INAKUA KWA KASI SANA NA TUNAWAOMBA WASOMAJI NA WADAU WOTE KUWEZA KUSHIRIKIANA NA LUKAZA BLOG KATIKA KUHAKIKISHA JAMII INAYOTUZUNGUKA INA PATA FAIDA KUPITIA MTANDAO HUU KWA KUFANYA KAZI PAMOJA. TUNAJUA KUWA NI VIGUMU KUMRIDHISHA KILA MTU LAKINI TUTAJITAHIDI KADRI YA UWEZO WETU KATIKA KUHAKIKISHA JAMII INAPATA HABARI HUSIKA KATIKA MUDA HUSIKA.

LUKAZA BLOG ILIANZA IKIWA NA MFANYAKAZI MMOJA TU AMBAYE NDIO MMILIKI WA MTANDAO HUU LAKINI NASHUKURU MTANDAO HUU UNATIMIZA MIAKA 2 UKIWA NA WAFANYAKAZI WAPATAO WAWILI MPAKA SASA HAYA NI MAENDELEO KWA MTANDAO HUU UKILINGANISHA NA ULIVYOANZA.

NACHUKUA FURSA HII KUWASHUKURU WADAU WOTE  KUANZIA WASOMAJI, BLOGGERS WENZANGU,MAKAMPUNI YANAYOFANYA KAZI NA LUKAZA BLOG KAMA VILE  KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI KWA KUWEZA KUFANYA KAZI NA MTANDAO HUU PIA NIWASHUKURU BENKI YA NMB PIA KWA KUFANYA KAZI NA LUKAZA BLOG AMBAPO KWA KIASI KIKUBWA WAMESAIDIA MTANDAO HUU KUFIKA HAPA ULIPO.

NINA MENGI YA KUANDIKA NA HATA NIKIENDELEA KUANDIKA HAPA NADHANI NAWEZA KUJAZA NAFASI NA BADO NISIMALIZE

PIA NAPENDA KUISHUKURU TIMU NZIMA YA LUKAZA BLOG  KWA KUWEZA KUFANYA KAZI NA MTANDAO HUU KWA MOYO MMOJA NA KWA UAMINIFU WA HALI YA JUU.

VILEVILE NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII KUWASHUKURU WASOMAJI WANGU,BLOGGERS WENZANGU NA WADAU WOTE NA WITO WANGU NI KUWAOMBA KUENDELEA KUSHIRIKIANA VIZURI KATIKA KULETA MAENDELEO YA TASNIA HII.

NAWAPENDA WOTE NA NAWATAKIA SIKU NJEMA NA KAZI NJEMA
MWISHO KABISA NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII KUKARIBISHA MAKAMPUNI,WATU BINAFSI NA MASHIRIKA MBALIMBALI KUWEZA KUTANGAZA BIDHAA ZAO NA HUDUMA ZAO HAPA KWA BEI NAFUU KABISA NA KUPATA MAFANIKIO YA BIASHARA YAKO KUPITIA MTANDAO HUU.

Ahsante sana Na Sina jinsi ya Kuwalipa maana fadhila zenu ni Nyingi lakini Mungu Atawalipia na kuwazidishia Mara mbili ya Kile Mlichokitoa katika Kufanikisha Lukaza Blog kupata mafanikio haya madogo.


Mungu Awabariki, Awajalie na Awazidishie.

KUPERUZI LIBENEKE LA LUKAZA BLOG BOFYA HAPA 

UKIWA NA TAARIFA,HABARI UNAWEZA KUTUTUMIA KUPITIA BARUA PEPE HII josephat.lukaza@gmail.com na sisi tutaiotoa kama ilivyo na ni bure kabisa.

- JOSEPHAT LUKAZA -
- LUKAZA BLOG-
- 0712 390 200 -
- josephat.lukaza@gmail.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...