Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 27, 2012

RASHID MATUMLA NA PATRICK AMOT WA MKENYA KUZICHAPA KESHO MTWARA, WAPIMA UZITO LEO Bondia Rashid Matumla na Patrik Amot wa kenya wanategemea kupanda ulingoni kesho katika ukumbi wa makonde mkoani mtwara.

Mabondia wote wamepima na kuwa na afya njema na wote kuwa katika uzani sawa wa kilo 73 kila mmoja.zoezi zima la upimaji liloendeshwa na katibu mkuu wa TPBO Ibrahim Kamwe na Dkt. Madono lilienda vema.
 
Pia katika pambano hilo kutakuwa na mapambano ya utangulii kati ya Bakari Mohamed wa Mtwara na Abdallah Mohamed wa Dar es Salaam, katika pambano la ubingwa kg57.

Aidha kutakuwa na mapambano mengine mengi ya utangulizi kati ya mabondia kutoka Black Mamba ya Mtwara na mabondia kutoka jijini Dar es Salaam, kama Haruna Mnyalukolo, ambaye atacheza na Ashraf Abdallah, Issa Matumla (mtoto wa Rashid Matumla) atacheza na Hamis Mtupeni, Hamis Ali Mkupa wa Mtwara atacheza na Ide Mnali katika pambano la raundi nane.
Mabondia wakiendelea na zoezi la kupima uzito, leo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...