Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, October 29, 2012

TWIGA CEMENT YAKABIDHI ZWADI KWA WASHINDI WA TUZO ZA MAZINGIRA


  Mkurugenzi Idara ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ignace Mchallo (kushoto) akimpongeza  Leonard Gastory Lugali, akiyeibuka mshindi wa kwanza wa shindano kuhusu  mazingira lililopewa jina la‘Quarry Life Award’ lililokuwa likiendeshwa na Kampuni ya Saruji yaTanzania Portland Cement (Twiga) na kupewa zawadi ya EURO 5000 katika hafla iliyofanyika kiwandani hapo, Dar es Salaam jana. Mshindi wa pili alipewa EURO 5000 na wa tatu aliondoka na 1500. Wengine pichani washindi, majaji wa shindano na maofisa wa TPCC.
  Mkurugenzi Idara ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ignace Mchallo (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya Euro 3000 kwa David Dawson Maleko,akiyeibuka mshindi wa pili wa shindano kuhusu  mazingira lililopewa jina la ‘Quarry Life Award’ lililokuwa likiendeshwa na Kampuni ya Saruji ya Tanzania Portland Cement (Twiga) katika hafla iliyofanyika kiwandani hapo, Dar es Salaam jana.  Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa TPCC, Ignatius Asare, , Ofisa Mazingira, David Mwakalobo, Meneja Mazingira wa Twiga, Juliet Mboneko Tibaijuka  na Meneja Mazingira kutoka HeidelbergCement, Dk Michael Rademacher.
 Washindi wa tuzo za Quarry Life Award wakipozi na tuzo zao kutoka kushoto ni, Leonard Gastory Lugali (mshindi wa kwanza), David Dawson Maleko (mshindi wa pili) na Kelvin Ngongolo, mshindi wa tatu.
Mkurugenzi Idara ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ignace Mchallo (kushoto) akikabidhi cheti kwa Meneja Mazingira wa TPCC, Juliet Mboneko Tibaijuka, mmoa wa watu waliofanikisha mchakato wa tuzo hizo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...