Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 24, 2012

NBC yawazawadia washindi wa Promosheni ya 'Dabo Mshiko'Meneja wa Tawi la NBC Mnazi Mmoja, Judith Motta (kulia) akikabidhi zawadi ya fedha taslimu kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya Dabo Mshiko wako na NBC, Kidaki Ndege Sospeter jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Chapa na Matangazo wa NBC, Arden Kitomari.

Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Chang’ombe, Blessing Kijalo (kulia) akikabidhi zawadi ya fedha taslimu kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya Dabo Mshiko wako na NBC, Joseph Saindani Nyilenda jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Chapa na Matangazo wa NBC, Arden Kitomari.

Mmoja wa washindi wa promosheni ya Dabo Mshiko wako na NBC,Joseph Saindani Nyilenda akionyesha zawadi yake ya fedha taslimu mara baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam.

Mshauri wa Mahusiano wa Benki ya NBC, Eddie Mhina akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa promosheni ya Dabo Mshiko wako na NBC jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...