Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, October 22, 2012

Wateja wa Barclays kushuhudia Ligi Kuu ya England (BPL) live


Mkuu wa Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Towo Kavishe (kushoto) akionyesha jezi halisi ya timu ya Arsenal ikiwa ni moja ya zawadi watakazopewa washindi wa promosheni ya Ligi Kuu ya England (BPL) inayoendeshwa na benki hiyo. Mshindi mmoja katika kila droo hujishindia tiketi ya yeye na mwenzake kwenda kushuhudia moja ya mechi ya ligi hiyo nchini Uingereza. Droo hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Maggid Bakari na Mkuu wa Bidhaa, Huduma na Utafiti wa benki hiyo, Samwel Mkuyu.
Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Rukia Kizwi (kushoto) akitoa tiketi ili kumpata mmoja wa washindi wa promosheni ya Ligi Kuu ya England (BPL) inayoendeshwa na benki hiyo. Mshindi mmoja katika kila droo hujishindia tiketi ya yeye na mwenzake kwenda kushuhudia moja ya mechi ya ligi hiyo nchini Uingereza na wengine wawili hujishindia zawadi ndogondogo. Droo hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano wa Barclays, Tunu Towo Kavishe, Mkuu wa Bidhaa, Huduma na Utafiti wa benki hiyo, Samwel Mkuyu, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakari Maggid na Ofisa Mawasiliano wa Barlclays, Lilian Machare.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...