Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 30, 2012

CUF YAOMBA OPERESHENI YA KUWAKAMATA WAHALIFU IFANYIKE KITAALAMU


Mkurugenzi wa Haki za Binadamu CUF Salim Bimani akifafanua jambo kupitia Katiba katika mkutano wake wa kupinga matumizi mabaya ya Operesheni inayofanywa na Jeshi la Polisi na Vikosi vya SMZ kuwatafuta wavunjifu wa amani.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
 ……………………………………….
Chama cha Wananchi CUF kimeliomba Jeshi la Polisi Zanzíbar kutumia mbinu za kitaalamu katika kuwasaka na kuwakamata watu wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya uvunjifu wa amani katika ghasia zilizotokea karibuni ambazo pia zilisababisha kuuliwa kwa Koplo wa Polisi Said Abdulrahman.
 CUF kimelishauri Jeshi hilo pamoja na Vikosi vya SMZ kuacha kuvamia makazi ya wananchi, na kuwaadhibu kwa vipigo kwa madai ya kutekeleza Operesheni ya kuwatafuta wahalifu wa matokeo hayo.
 Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Vuga,Mkurugenzi wa Haki za Binadamu CUF Salim Bimani amesema Operesheni ya kutumia uvamizi bila kutumia njia za kitaalamu za kutafuta wahalifu zinakuza mgogoro uliopo badala ya kuupunguza.
 Amesema matendo ya uvunjifu wa Amani na kuuliwa kwa Koplo Said Abdulrahman yanafanana na matukio ya uvunjifu wa amani Tanzani Bara lakini Jeshi la Polisi Bara limekuwa likitumia njia za kitaalamu katika kuwakamata wahalifu bila raia wengine wasio na makosa kuathirika na Operesheni hiyo.
 Ametoa mfano wa kuuliwa kwa Kamanda wa Polisi Mwanza Liberatus Barlow na matukio ya uvunjifu wa amani Dar es Salaam ambapo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vikosi vya ulinzi viliweza kutuliza hali hiyo na kufanikiwa kuwakamata wahusika na kupelekwa mahakani bila hata kuwaathiri wanachi ambao hawakuhusika na kadhia hiyo.
 Ameongeza kuwa Mahala popote panapohitajika kufanywa Operesheni ya kuwasaka wahalifu mamlaka husika ndizo zinazobeba dhamana na jukumu la kutumia uataalamu,mafunzo na mbinu zinazoepusha ukiukwaji wa haki za binadamu na hatimaye kufanikisha lengo.
 Bimani ameongeza kuwa CUF inalaani kwa nguvu zote vitendo vya fujo na uvunjifu wa amani vilivyofanyika Octoba 17 hadi 19 vikijumuisha mauaji ya Koplo Said, Salim Hassan Mahaju na Hamadi Ali Kaimu ambao wote waliuawa kutokana na fujo hizo. 
 Kwa upande wao baadhi ya wananchi ambao waliathirika na fujo hizo wameiomba Serikali kuingilia kati operesheni hiyo na kutaka kutafutwe njia stahiki za kuwakamata wahalifu bila ya kuwapiga au kuwanyanyasa ambao hawahusika na fujo hizo.
 Wamedai kuwa tokea kuanzishwa kwa Operesheni hiyo wamekuwa hawana muda wa kujishughulisha na kazi zao za kutafuta riziki badala yake wamekuwa wakijifungia nyumbani mwao ili kujinusuru na vipigo.
 Katika maeneo ambayo Operesheni hiyo imekuwa ikifanywa mara kwa mara ni Bububu, Amani, Magogoni, Daraja bovu, Mwanakwerekwe,Mtoni,Kinuni,Mboriborini,Mikunguni na Kwarara.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...