Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, October 29, 2012

Diamond Platnum akibeba kilio cha Dallas wa Wolper(Dallas)
Dallas aliyejipatia jina fasta fasta katika jiji la Dar es salaam kutokana na utumiaji wa fedha ambao ulivuka mpaka wa matumizi na kuonga vitu vya thamani kwa mwanadada wa Bongo Movie Jackline Wolper,
amemnunua mwanamuziki Diamond kwa kumpa fedha za kwenda kurekodi wimbo mmoja pamoja na video ambayo inaelezea maisha yake ya mwanadada huyo ilikumponguza ukali wa machungu aliyokuwa nayo. Habari zikiwa bado za motomoto kutoka kwake mwenyewe Dallas, alisema video ya wimbo huo ambao kuna uwezekano ukaitwa Mapenzi sasa Basi, itafanyika nchi za Kiarabu.
Utamu zaidi unaeleza kwamba Dallas alimchukuwa Diamond hadi Dubai kwaajili yakuangalia Location huku akijinadi kwamba haiwezi kufanyiwa Coco Beach. Alizidi kueleza kwamba machungu ya moyo wake yote aliamua kuyamwaga katika wimbo huo, ambapo kila anpousikiliza unapopigwa basi anajikuta akilalamika na kusema 'Mimi mapenzi basi'.
Wimbo huo hata hivyo bado haujaachiwa lakini wadau tayari wameshaweza kuusikiliza na kuutamani kuona hiyo video yaani, kwa jinsi wimbo huo ulivyokuwa dipu katika mapeniz huku kijana Naseeb Abdul 'Diamond' akisikitikia mapenzi kwa niaba ya Dallas.


(Jack Wolper ezi hizo akitanua na mali za Dallas)
 
Hizi ni baadhi ya picha ambazo zimefanyiwa Auddition ya video hiyo mpya.No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...