Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 30, 2012

MSONDO NGOMA YATANGAZA RATIBA YA WIKI



BENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania, Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ imetoa ratiba yao katika wiki baada ya mpambano wao mkali na mahasimu wao Sikinde uliofanyika Jijini Dar es salaam pamoja na Zanzibar baada ya kutoa burudani ya Iddi sasa wamerudi kwa ajiri ya kutoa burudani  ambapo wamesema kuwa wataanza kutoa burudani siku ya Ijumaa watakuwa Leanders Club Kinondoni, Jumamosiwatakuwa  Kilim
ani Pub Staki Shari, na jumapili watamariza wiki endi katika Ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni

Akiongea , Msemaji wa Msondo, Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa wameamua kutoa ratiba hiyo ili mashabiki wao waweze kujua nini kinachoendelea baada ya kusherekea sikukuu .

“Msondo ipo kamili katika kutoa burudan na ndiyo maana imeamua kutoa ratiba, hivyo tunaamini mashabiki wetu watakuja kwenye matamasha yetu kwani bila wao sisi hatuwezi kusimama na kuimba,” alisema Super D.

Alitaja vibao vinavyotamba kwa sasa vya bendi hiyo kuwa na Suluhu wa Sabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa Eddo Sanga mbali na nyimbo hizo bendi hiyo itapiga nyimbo zake zilizotamba zamani zikiwemo Asha Mwanasefu,Cheusi Mangara,mwana Mkiwa na nyingine nyingi zilizotamba kipindi hicho

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...