Washiriki
wa mpango wa Mama Shujaa wa Chakula wakiwa katika picha ya pamoja na
Maafisa wa benki ya NMB tawi la Mbezi walipo tembelea tawi hilo.
Washiriki wa mpango wa Mama Shujaa wa Chakula wakipata mafunzo kutoka kwa Afisa wa Benki ya NMB tawi la Mbezi.
…………………………………………
Washiriki wa mpango wa Mama Shujaa
wa chakula unaodhaminiwa na benki ya NMB wametembelea tawi la NMB
Mbezi na kuonyeshwa jinsi NMB inavyoendesha shughuli zake za kibenki
katika matawi yake.
Washiriki hao waliongia katika
kijiji cha Maisha Plus hivi karibuni, vilevile walipata fursa ya kupata
elimu ya kifedha kupitia mpango wa NMB Financial Fitness.
NMB kupitia mpango wa NMB
Financial Fitness unaolenga kuongeza uelewa wa matumizi mazuri ya fedha
iliwaelimisha washiriki kuhusu huduma za kifedha, uwekaji akiba, kupanga
matumizi, matumizi mazuri ya kifedha na mengine mengi.
Vilevile, Washiriki hao walielimishwa kuhusu Mikopo Midogo na kati ya kibiashara pamoja na mikopo ya kilimo.
NMB inaamini udhamini huo ni
sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo
katika maisha, mapambano dhidi ya njaa,umasikini na uhaba wa ajira
miongoni mwa wanawake.
No comments:
Post a Comment