MAHAKAMA Kuu Kanda Maalum ya Dar es Salaam leo imemwachia
huru Rais wa zamani wa Chama cha Ngumi za Ridhaa nchini (BFT), Alhaj Shaaban
Mintanga aliyekuwa akikabiliwa na shitaka la kula njama na kusafirisha
dawa za kulevya zenye uzito wa Kilo 4.8 kutoka Tanzania kwenda Mauritius baada
ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo.
Akitoa hukumu hiyo leo, Jaji wa Mahakama hiyo, Twalib Fauz, alisema upande wa
mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka hayo hivyo kumuachia huru
mshitakiwa huyo.
Mintanga alikamatwa Aprili 4, 2008 nchini Mauritius ambako
alikwenda na Timu ya Taifa Ngumi za Ridhaa akiwa kiongozi. Mara baada ya
kukamatwa na madawa hayo alishitakiwa na kurejeshwa nchini ambako alifunguliwa
kesi iliyodumu kwa muda wa miaka minne ambapo ameachiwa huru leo.
Katika kipindi chote cha kesi hii haikuwahi kusikilizwa hata
mara moja zaidi ya kuahirishwa kila ilipotajwa, hali iliyofanya mtuhumiwa
kudhoofika kiafya kutokana na hali aliyokuwa nayo huko gerezani. Mwenendo
wa kesi hiyo uliwafanya baadhi ya wadau kuona kama kulikuwa na mkono wa mtu
wenye lengo la kumkomoa.
Mintanga
ambaye ni muumini mzuri wa dini ya Kiislamu aliyewahi kwenda kuhiji Maka mara
baada ya hukumu hiyo ya kuachiwa huru, alionekana kutabasamu na hakupenda
kuzungumza chochote na vyombo vya habari bali alikwenda kwenye moja ya vyumba
vya mahakama na kukaa huko.
Mpaka mtandao huu unaondoka mahakamani, Mintanga alikuwa hajaondoka katika
chumba hicho.
|
No comments:
Post a Comment