Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 22, 2013

Abdi Kassim ‘Babi’ atua KMKM ya ZenjiKiungo wa zamani wa Yanga na Azam, Abdi Kassim ‘Babi’ amejiunga na mabingwa wa Zanzibar, Kikosi Maalum Kuzuia Magendo (KMKM).
Babi ambaye msimu uliopita aliichezea Azam lakini aliachana na klabu hiyo baada ya kukataa kuongeza mkataba mwingine, aliambia kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa amejiunga na timu hiyo jana bila kutaja dau alilosajili wala urefu wa mkataba wake.
Kiungo huyo ambaye pia alicheza soka la kulipwa nchini Vietnam aliandika katika uikurasa wake kuwashukuru viongozi wa KMKM kwa kufanikiwa usajili wake na ana furaha kuitumikia timu hiyo katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Zanzibar.
Babi ambaye pia huitwa Barrack wa Unguja aliandika maneno yafuatayo,
“hi nyote ...nashukuru Mungu mzima wa afya ...nimesaini mkataba na KMKM, mabingwa wa soka Zanzibar na timu inayoshiriki mashindano ya kimataifa na mashindano mbalimbali.
“...ikiongozwa na kocha mzoefu na mwenye ujuzi wa hali ya juu, Ali Bushir ...so natoa shukrani za dhati kwa uongozi wa KMKM kwa kumaliza zoezi la usajili kati yangu na wao na napenda kuwashukuru wapenzi wa KMKM kwa kuniunga mkono.
“Nafurahi zaidi kwa vile nipo nyumbani na familia yangu na biashara zangu za hapa na pale...asanten sana watanzania wote.”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...