Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, August 14, 2013

WLADIMIR KLITSCHKO KUMVAA ALEXANDER POVETKIN OKTOBA 15 MOSCOW, Russia


BINGWA wa masumbwi duniani katika uzani wa WBA, Wladimir Klitschko (pichani), anatarajia kupanda ulingoni kumvaa bondia asiyepigika raia wa Russia, Alexander Povetkin.

Pambano baina ya miamba hiyo ya 'ndonga' linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo huo duniani, litapigwa jijini hapa Oktoba 5.

Huo utakuwa utetezi wa kwanza kwa Klitschko, dhidi ya nkali huyo wa masumbwi raia wa Russia, ingawa mazungumzo ya mkataba wa mtanange huo hayajafikia tamati.
"Tunaweza kukutana mapema iwezekanavyo," alisema Klitschko na kuongeza; "Hajawahi kupoteza pambano lolote na katika hilo hakuna tatizo kwangu, kwani namfahamu vema."
Kwa upande wake Povetkin alisema: "Nina furaha kama pambano hilo litakuwepo. Mimi naangalia mbele katika kukuktana na bondia huyo imara ulingoni."
Wakati Klitschko, 37, ana rekodi ya kupanda ulingoni katika mapambano 63 na kushinda mara 60, yakiwamo 52 ya KO, Povetkin ana rekodi ya kushinda mapambano yake yote 26, yakiwamo 18 ya KO.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...