Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 16, 2013

FILAMU YA DOUBLE J KUJA KIVINGINE NA MASTAA KIBAO WA FILAMU


ANGEL MAGIGE na KhalidRamandhani Dogo ni miongoni
mwa nyota wapya waliofanya vizuri  ndani ya sinema
mpya iitwayo Doble J.


Muongozaji na muigizaji  kinara wa filamu hiyo,
Jimmy Mponda jimmy Master  au J Plus ameeleza kuwa
muda si mrefu filamu ya Doble J sehemu ya mwisho
itaingia sokoni.

Mapema wiki iliyopita wakati akizungumzia filamu
 hiyo, J Plus aliyetamba na mfululizo wa filamu za
Misukosuko 1,11 na 111 ,alisema sehemu ya kwanza , ya
pili na ya tatu ya Doble J ilitoka mwaka jana.


Alieleza kuwa ndani ya filamu hiyo ,Angel ameigiza  kama
mtumiaji wa dawa za kulevya  akitumia jina la Kwapu.

'Koku na Kwapuwamefanya poa sana kwenye ujio huo wa Doble J
Final, mashabiki wangu wajiandae kuipata sehemu ya mwisho
ili waone nini kilitokea,"alisema J Pulus.

Ndani ya ujio huo wa mwisho waigizaji kama Seleh Juma 'Pwicho'
,Ibrahim Mbwana 'Bad Boy'  na nyota wengine  ni Charles Magari,
Hashimu Kambi naVeronica Viankero.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...