Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 22, 2013

'DOGO' WA SIR NATURE ASIKIKA REDIONI


Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na kazi yake inayojulikana kwa jina la ‘Haipotei’, msanii wa muziki wa bongo fleva, Juma Kassim ‘ Sir Juma Nature’, anatarajiwa kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Dogo’ hivi karibuni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Sir Nature alisema ngoma hiyo ameikamirisha na yupo katika hatua za mwisho za kuanza kuisambaza kazi hiyo.

“Kazi hii imekamilika, kilichobaki ni kuisambaza katika vituo mbalimbali vya radio na kwa wale wanaotaka kuisikiliza, kuanzia kesho tembelea kwenye blog ya tmkwanaumehalisi utaisikiliza kupitia humo na utatupia ‘comment’ yako na maoni yako kuhusu kazi hiyo,” alisema.

Aliwaomba samahani mashabiki wake kwa kukaa kimya muda mrefu na kuongeza kuwa, baada ya kuisambaza kazi hiyo katika vituo mbalimbali vya radio ataanza maandalizi ya video muda wowote.


Licha ya kuandika kwenye facebook kuwa ngoma hiyo ingesikika wiki iliyopita, Nature amesema hakuweza kufanya hivyo kutokana na majukumu, hivyo siku yoyote kuanzia leo ataisambaza katika vituo mbalimbali vya redio.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...