Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 20, 2013

BANZA STONE ATIMULIWA EXTRA BONGO


Banza Stone.
***************************************
UONGOZI wa bendi ya muziki wa dansi Extra Bongo 'Next Level Wazee wa 
Kizigo' umemfungulia mlango wa kutokea mwimbaji wake mahiri Ramadhani Masanja 'Banza Stone' kuwa yuko huru kujiunga na bendi yoyote anayoamini ndio hitajio lake kwa sasa.

Kauli ya Extra Bongo imekuja siku chache baada ya mwanamuziki huyo, Banza kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kukacha kuhudhuria baadhi ya maonyesho ya bendi hiyo  huku akionekana kwenye jukwaa la moja ya bendi maarufu ya muziki wa dansi nchini ambayo ni wapinzani wa 'Wazee wa Kizigo'.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa bendi hiyo, 'Kamarade' Ally Choki, amefanya jitihada za kila aina kumjenga kisaikolojia mwanamuziki huyo aweze kujitambua wapi alikotoka na alipo sasa lakini sasa amesema inaelekea Banza ni sikio la kufa lisilosikia dawa.

"Yako mambo mengi ambayo amekuwa akiyafanya,  kama bendi tumekuwa tukikwazika nayo lakini tunafanya jitihada za kumrudisha kundini kwa kumshauri lakini mwenzetu amekuwa tofauti hivyo kama amepata mahala anakoamini ndiko kutamuwezesha kutimiza safari yake ya kimuziki ruksa kwenda,"alisma Choki.

Aidha,Choki alisema, baadhi ya vitendo vinavyofanywa na mwanamuziki huyo havipaswi kufanywa na staa kama yeye kwakuwa haziwapi mafunzo baadhi ya wanamuziki chipukizi waliomo ndani ya Extra Bongo lakini mbaya zaidi vimekuwa vikididimiza kipaji chake alichojaaliwa na muumba.

Alieleza Extra Bongo ni chuo cha muziki ambacho mipango yake ya muda mrefu ni kuinua vipaji vya wanamuziki chipukizi na kuwandeleza kwa kuwapa nafasi ya kuimba na kutunga kama ambavyo jahazi la bendi hiyo linaendelea kutesa chini ya mwamvuli wa vijana waliopo sasa ambao wameonyesha uwezo mkubwa.

Hata hivyo Mtandao huu umenasa habari za chini ya Kapeti kuwa Mwanamuziki huyo, hivi sasa anafanya mipango ya kurejea katika Jukwaa la Bendi ya Twanga Pepeta, ambapo mara kadhaa amekuwa akionekana katika maonyesho ya bendi hiyo, akipanda na kuimba wakati muda mwingine bendi yake ikiwa na shoo pia sehemu nyingine.

3 comments:

  1. mimi ni mdau wa Extra Bongo muda mrefu ila siku za karibuni nimeshindwa kuhudhuria shoo baada ya kutomuona Kabatano kwenye Satge na nasikia mmemsimamisha kazi rapa Kabatano!!!! haya yana ukweli? kiukweli kumsimamisha ni sawa na kuua Band mi nawashauri kama ana mapungufu jaribuni Kumuweka chini ili arejee kundini ahsante.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...