Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 22, 2013

AIRTEL MONEY YATIKISA MITAA YA JIJI LA DAR ES SALAAM

 

 Mkurugenzi Mkuu wa Airtel  Bw Sunil Colaso akiwashukuru watanzania kwa kutumia huduma za Airtel  wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea sokoni na kupeleka kwa watanzania promosheni ya Airtel money Hakatwi mtu hapa.
 Afisa kitengo cha rasilimali watu Airtel Tanzania bi Josephine Kajembe akiongea na wateja  juu ya huduma ya Airtel money yatosha na promosheni ya Airtel money Hakatwi mtu hapa wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea wateja sokoni katika maeneo mbalimbali jijini Dar es saalam
 
Wafanyakazi wa Airtel wakijipanga tayari kuingia sokoni na kuitambulisha promosheni ya Airtel money Yatosha  na kutoa elimu juu ya huduma zake hususani Airtel money kwa watanzania jijini Dar es Saalam.
Mkurugenzi wa mawasiliano Bi Beatrice Singano Mallya  akiongea na watanzania juu ya huduma ya Airtel money yatosha wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea sokoni na kupeleka kwa watanzania promosheni ya Airtel money Hakatwi mtu hapa.
...................................................................................................................................
Wananchi katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam leo wamepokea kwa kishindo promosheni ya Airtel money yatosha inayofahamika kwa jina la Hakatwi mtu hapa kwenye mitaa mbalimbali ya jiji hilo
Promosheni hiyo ilipokelewa kwa kishindo baada ya wafanyakazi wa Airtel kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaa na kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali na kuitambulisha rasmi sokoni promosheni ya Airtel money yatosha hakatwi mtu hapa 
Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Tandika wilaya ya Temeke walisema kuwa huduma hiyo ya Airtel money Hakatwi mtu hapa imeweza kurahisisha baadhi ya kazi zao na kuwawezesha kuhifadhi kiasi flani cha fedha ambacho awali kilikuwa kinakatwa kutokana na kutuma na kutoa pesa.
“Katika biashara zangu mimi huwa natuma na kupokea pesa mara nyingi tu, lakini awali nilikuwa nakatwa kiasi flani cha pesa ambacho mtu mwingine anaweza akaona kidogo lakini si kidogo ni kikubwa sana. Naishukuru Airtel kwa huduma hii ya Hakatwi mtu maana inanisaidia kiuchumi pale ninapotuma na kupokea pesa bure,” alisema Said Mrisho mfanyabiashara ndogondogo katika soko la Tandika.
Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso alisema “ Airtel tunawajali wateja wetu na kwetu mteja ni namba moja na ndio maana kwa mara nyingine tena wafanyakazi wote wa Airtel leo wanaingia sokoni ili kutoa elimu na kuwaelimisha watanzania na wateja wetu juu ya huduma zetu haswahaswa promosheni maalumu ya Hakatwi mtu hapa .
Tunazo huduma nyingine nyingi ambazo tunazitoa kwa wateja wetu kama vile Data 3.75G, Airtel Yatosha , na Huduma ya Airtel money ambayo sasa tunaendelea kuiboresha zaidi na kuwapa wateja wetu fulsa ya kutuma na kupokea pesa bure bila makato yoyote.
Lengo letu ni kuhakikisha Airtel inaendelea kutoa huduma zilizo na ubunifu, za kisasa zinazokithi mahitaji ya wateja wake na tunaamini Airtel money hakatwi mtu ni suluhisho sahihi na litaleta unafuu katika huduma za kifedha nchini 
Akizungumza katika ziara Mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano Bi Beatrice Singano alisema” watu wameonesha muitikio mkubwa sana katika kuipokea huduma yetu ya Airtel money hususani promosheni ya Airtel money Hakatwi mtu  na hiyo inaonesha wazi ni jinsi gani Airtel inavyotoa huduma zilizo bora na zinazokubalika kwa wateja wake na jamii nzima kiujumla.
“Promosheni hii ya Hakatwi mtu hapa inawawezesha mtu kutuma na kupokea pesa bure, yaani bila makato yoyote hivyo nachukua fulsa hii kuwahimiza watanzania kutumia huduma zetu za Airtel money ambazo ni rahisi , salama na zinapatikana nchi nzima 
Ili kutumia huduma ya Airtel money mteja anatakiwa kupiga *150*60# na kuunganishwa moja kwa moja na menu ya Airtel money kisha kufanya miamala mbalilimbali ikiwemo kutuma pesa, kulipa bill, kuongeza salio kununua LUKU, USA visa na nyingine nyingi. Aliongeza Singano.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...