Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 19, 2013

FOOLISH AGE YA LULU KUZINDULIWA MWISHO WA MWEZI HUU NDANI YA MLIMANI CITY DAR


Msanii mwenye kipaji cha Hali ya juu nchini na Mwenye umri mdogo Elizabeth Michael "LULU"anatarajia kuzindua filamu yake ya Kwanza tokea alipotoka Gerezani, Filamu hii iitwayo FOOLISH AGE ikiwa imetengezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited itazinduliwa Mnamo tarehe 30 August 2013 Katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam. 

Filamu hiyo inayoelezea Maisha ya LULU ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu kutokana na Kutengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited Katika Uzinduzi huo wa Filamu hiyo ya Lulu Wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi Band anatarajiwa kushusha bonge moja la burudani ya kufa mtu. 

Kupitia mtandao wa kijamii wa Lulu aliyejaaliwa kuwa na kipaji cha kuigiza na mwenye mvuto mbele ya runinga aliandika "Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu....!!!ninafuraha ya kuwafahamisha kuwa TAREHE 30/8/2013 ndio siku nitakayozindua movie yangu mpya iitwayo FOOLISH AGE....Hatimaye narudi kazini!!!!Uzinduzi utafanyika katika ukumbi wa MLIMANI CITY....kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa muziki....na pia LADY JAY DEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo pia!!!nahitaji support ya mashabiki wote wa LULU na mashabiki wa BONGO MOVIE.....♥♥♥♥!!!#PROINPROMOTERS"
Baada ya uzinduzi wa Filamu hii nakala zitaendelea kuuzwa katika maduka yote ya Filamu nchini na Filamu hii imetengenezwa na itakuwa inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited
Usikose uzinduzi Huu utakaofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City tarehe 30 August 2013

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...