Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 23, 2013

Washiriki Epiq BSS kuingia kambini


 Jaji Mkuu wa shindano la kuimba la Epiq BSS, Ritha Paulsen, akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya shindano hilo. Anayemfuatia ni meneja wa vipindi wa TBC, Edna Rajab na Walter Chillambo, mshindi wa shindano hilo mwaka jana.
Mshiriki wa shindino la kuimba la Epiq BSS, Menina Atick ambaye aliingia kwa njia ya usaili wa simu, akimkabidhi jaji mkuu wa shindano hilo Ritha Paulsen video ya wimbo wake.

·        Inaonyeshwa TBC Taifa Jumapili saa tatu usiku na kurudiwa jumatano saa 8
·        Imepata mafanikio makubwa mikoani
·        Usaili kwa njia ya simu unaendelea
Dar es Salaam, 21-8-2013: Shindano la kuimba la Epiq BSS limetangaza kuwaingiza washiriki wake waliongia 20 bora kambini, ili waanze mafunzo mapema na kutoa washiriki bora zaidi mwaka huu.
Shindano hilo ambalo kwa mwaka huu linarushiwa kwenye kituo cha televisheni cha TBC, kila Jumapili saa tatu usiku na kurudiwa kila jumatano saa nane mchana, limevuta mashabiki wengi nchini kwa burudani wanayoipata.

‘Mwaka huu washiriki waliongia ishirini bora wataingia kambini mapema zaidi, ili kuhakikisha wanajifunza mambo mengi, hali itakayoleta ushindani zaidi pamoja na kuzalisha washiriki ambao watafanya vizuri kwenye soko’ alisema Ritha.

Ritha pia amefurahishwa na mafanikio makubwa ambayo Epiq BSS limepata mikoani, kwa idadi nzuri ya vijana waliojitokeza lakini pia ubora wa vipaji vilivyojitokeza.

“Tumepata washiriki mahiri kutoka mikoa mbalimbali,hivyo mashindano ya mwaka huu yatakuwa na ushindani mkali sana na ninaamini tutapata wasanii bora zaidi kuliko miaka iliyopita” alisisitiza Ritha.

Kwa upande wake Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, alisema kampuni yake imedhamiria kuboresha shindano hilo mwaka huu kwa kuongeza vitu mbalimbali.

‘Kwa hakika tumefanikiwa kuboresha shindano kwa kiasi kikubwa, lakini pia tumehakikisha washiriki waliopita wanaendelea vizuri, mfano mzuri ni Walter na Menina ambao wanafanya vizuri kwenye soko’ alisema Khan.

Usaili wa Epiq Bongo Star Search kwa mwaka huu umefanyika katika mikoa sita ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Dodoma na kumalizia Dar es Salaam.

Washiriki 50 walipatikana kutoka mikoa yote, na wamechujwa na kubakia washiriki 20 ambao ndio watakao ingia kambini.
Washiriki wanaotaka kufanya usaili kwa njia ya simu wanapaswa kupiga namba 0901551000 au watume ujumbe mfupi kwenda 15530 kupata maelezo ya namna ya kujiunga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...