Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 20, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUADHIMISHA SIKU YA MABUNGE DUNIANI KUHUSU SUALA LA MAKAZI, JIJINI ARUSHA LEO Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. Kulia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Prof. Anna Tibaijuka. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Ukumbi wa Bunge la Afrika Mashariki, baada ya kufungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, lililofunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha
 
 Baadhi ya wabunge na wageni waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano hilo leo, jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Tree Ltd ya Arusha, Magdalena Ayo, kuhusu utengenezaji wa Majiko Bomba, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, lililofunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. 
Picha  ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...