Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 19, 2013

Mpango wa Taifa wa Damu salama wavuka lengo


 
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Bw. Rajab Mwenda akizungumza na waandishi wa habari jana kutoa takwimu za makusanyo ya damu kwa mwezi Aprili mpaka Juni mwaka huu ambapo ulivuka malengo kwa asilimia 111 kutoka chupa 36,278 mpaka 38,948. Kulia ni Ofisa Msaidizi wa Masoko na Uhusiano Bi. Rayah Hamad  (Picha na Mpiga picha maalum).
                                  

                                                      PRESS RELEASE                           
MPANGO wa Taifa wa Damu Salama umevuka lengo la makusanyo ya damu katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu kwa kukusanya chupa za damu 38,948 ambazo ni asilimia 111 ikilinganishwa na chupa 36,278 zilizokusanywa kutoka Januari hadi Machi mwaka huu.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Damu Salama, Bw. Rajab Mwenda akizungumza jana Dar es Salaam alisema kanda inayongoza kwa uchangiaji ni Mashariki na Kanda ya Ziwa.
Alisema mafanikio hayo yametokana na uanzishajiwa mpango wa damu salama wa  kampeni ya kuhamasisha uchangiaji damu kwa hiari  katika jamii na kushirikisha wadau.
 Bw. Mwenda alisema maadhimisho ya siku ya wachangia Damu duniani ambapo lengo la kukusanya chupa za Damu 8,500 kutoka kanda sita za mpango wa Taifa wa damu salama liliwekwa na mpango ulifanikiwa kukusanya jumla ya chupa 8,683
Alisema Mpango wa Damu salama kushirikiana na wadau mbalimbali kama asasi za kiraia  nayo imeongeza makusanyo ya damu toka vituo vidogo vya kuchangia damu Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,  Morogoro na Dodoma kutoka chupa za damu 2,560 mpaka chupa 3,151 kufikia Aprili hadi Juni mwaka huu.
 Aliwaomba wadau kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari kwa kutumia vyombo vya habari, mitandao ya jamii na vipeperushi.
Bw. Mwenda alisema ushirikiano ni mdogo kati ya wahamasishaji wa Mpango  wa damu salama na viongozi wa Taasisi mbalimbali, matumizi mabaya ya damu kidogo inayopatikana katika hospitali zetu na miundo mbinu hafifu hususan barabara mbovu wakati wa ukusanyaji  na usambazaji wa damu.
Alisema changamoto nyingine ni uuzwaji wa chupa za damu kunakofanywa na baadhi ya watumishi wa hospital ambao si waaminifu hivyo kukatisha tamaa wachangia damu kwa hiari.
Bw. Mwenda alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilianzisha Mpango wa Taifa wa Damu Salama mwaka 2005 ili kuhakikisha uwepo wa damu salama na ya kutosha kwa wote wanaohitaji.
Alisema shughuli za mpango ni pamoja na uhamasishaji jamii kuhusu uchangiaji damu wa hiari, ukusanyaji upimaji na usambazaji wa damu salama mahospitalini.
“Mpango wa Taifa wa Damu salama unafanya kazi kwa kushirikianana kitengo cha kuzuia magonjwa (CDC)  na wadau wengine wa Chama cha Msalaba Mwekundu na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)” alisema Bw. Mwenda.
Alisema Mpango wa Taifa wa Damu salama uliweka lengo la kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) katika damu iliyokusanywa asilimia 1.1 kwa kipindi Aprili- Juni ikilinganishwa na asilimia 1.2 kipindi cha Januari hadi Machi baada ya kujikita katika suala la uhamasishaji na kutoa damu toka kwa jamii ambayo ni salama, kuboresha dodoso la wachangiam damu na kuendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu na wachangiaji kujiepusha na tabia hatarishi ili wawe wachangiaji wa kujirudia.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...