Pichani ni sehemu ya paa la chumba cha habari cha chama cha mpira wa miguu Tanzania (TFF),ambacho
kinatumika kukutana na Wanahabari wa vyombo mbalimbali kuhusiana
tasnia ya michezo kwa madhumuni ya kuihabarisha jamii. Kwa wanahabari za
Michezo naamini kabisa mtakubaliana na mimi kuhusiana na hali iliyopo
ndani ya ofisi hiyo,ambayo kimsingi nayo una umuhimu wake mkubwa,lakini
imetelekezwa kama hivyo.
Chombo cha kutoa ubaridi ambacho kiliwekwa angalau kupunguza joto la
Daslam ofisini humo,lakini kwa sasa ndege wamepata mahala pa
kujipumzikia na kuzaliana,lakini sio ishu.
Taa nazo ziko hoi zinaning'inia tu,jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa watu.
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakisubiri wahusika wa
TFF,kukutana na Wanahabari hao kwa ajili ya kuwapa taarifa mbalimbali
za michezo,ili jamii ihabarishwe.
Dude la kuwekea Maji ya Kunywa ambalo sijui kwa mara ya mwisho lilitumika lini,kwani limejaa vumbi,haliangaliwi tena. zaiihttp://kajunason.blogspot.com/ |
No comments:
Post a Comment