Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) pamoja na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini
(TPBC) zimeidhinisha kufanyika kwa mapambano manne ya ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati
Ghuba ya Uarabu na Uajemi jijini Dar-Es-Salaam mwezi wa Novemba mwaka huu.
Mapambanohayoambayonimaraya kwanza kufanyika katika ukanda huu wa dunia yatakuwa yanashirikisha mabondia kutoka Misri,
Kenya, na Tanzania na yatarushwa live na televisheni za Tanzania, Kenya naMisri.
Kufanyika kwa mapambano haya kumewezekana baada ya makapuni manne kutoka
Tanzania na Misri kuungana na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF)
na kuanzisha programu ya mwaka mmoja itakayoanza Novemba mwaka huu hadi Novemba mwakani.
Katikaprogramuhiimakampunihayapamojana IBF yataandaa mapambano kila baada ya mwezi mmoja Novemba,
Januari, Machi, Mei, Julai, Septemba na Novemba mwakani.
Raiswa IBF katikabara la Afrika,
Masharikiya Kati,
Ghuba ya Uarabu na Uajemi Onesmo Ngowi aliyataja makampuni hayo kuwa ni pamoja na Jambo
Concept inayomiliki vyombo vya habari vikiwamo gazeti la Jambo Leo, Tanzanite Sports
Promotion Management, Kitwe General Traders yote ya Tanzania na Louaa Boxing
Promotion ya Misri.
Katikamapambanohayo, mabondia Alphonce
Joseph Mchumiatumbo atapambana na bondia wa Misri anayeishi nchini Marekani, Manzur Ali
katika uzito wajuu (Heavyweight) kugombania mkanda wa IBF Mashariki ya Kati,
Ghuba ya Uarabu na Uajemi na Afrika.
Bondia wa Misri, Mohammed Metually, ambaye ni bingwa wa Afrika anayetambuliwa na Baraza
la Ngumi la Dunia (WBC) atapambana na bondia Nofart Emilio, wa Kenya kugombea mkanda wa IBF
Mashariki ya Kati, Ghubaya Uarabu na Uajemi na Afrika katika uzito wa Bantam.
Naye bondia bora wa TASWA mwaka 2011 Nassibu Ramadhani, atachuana vikali na bondia asiyepigika,
Nick Otieno, wa Kenya kugombea mkanda wa IBF Mashariki ya Kati,
Ghuba ya Uarabu na Uajemi na Afrika katika uzito wa Super Flyweight.
Bondia anayepanda chati kwa kasi Haji Juma, kutoka viunga vya jiji
la Tanga atapambana na bondia Twalib Mubiru, wa Kenya kugombea mkanda wa IBF
Afrika katika uzito wa bantam.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania na bara la Afrika kuwa na mapambano mengi ya ubingwa wa
IBF kwa usiku mmoja.
Mabalozi wengi wanaoziwakilisha nchi zao hapa
Tanzania, wageni wengi wanaoishi Tanzania na wadau wengi wa ngumi kutoka Misri, Kenya,
Uganda na chi za jirani watahudhuria mapambano haya kwa maelfu.
Imetumwana:
Onesmo
Alfred McBride Ngowi
Rais,
IBF
Africa, Masharikiya Kati, GhubayaUarabunaUajemi
No comments:
Post a Comment