Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 12, 2012

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Bara la Afrika Akutana na Ujumbe Kutoka Tanzania Ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Gavana Wa Benki Kuu



Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu akitoa maoni yake  kwenye mkutano na Makamu wa Rais wa Dunia hayupo pichani hapa Jijini Tokyo- Japan.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. William Mgimwa akiwa na ujumbe katika mkutano, wa kwanza kulia ni Bi. Salome Sijaona ambaye ni Balozi nchini Japan akifuatiwa na Bw. Siyvacius B. Likwelile Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha akifuatiwa na Bw. Khamisi Mussa Omari Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar katika mkutano Jijini Tokyo- Japan.
Wa pili kutoka kulia ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia  kwa Bara la Afrika, Bw. Makhtar Diop,akiwa ameambatana na  Maafisa  Waandamizi kutoka Benki ya Dunia wakati wa mazungumzo na Waziri wa Fedha Mhe. William  Mgimwa hayupo kwenye picha.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia  kwa Bara la Afrika, Bw. Makhtar Diop,akifurahia jambo, wakati wa mazungumzo na Waziri wa Fedha Mhe. William  Mgimwa hayupo kwenye picha.
Waziri wa fedha Mhe. Mgimwa akifafanua jambo kwa Afisa wa Benki ya Dunia.
Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Mhe. Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa pamoja na maafisa kutoka Benki ya Dunia wakiendelea na majadiliano juu ya kuangalia uwezekano wa kuisaidia Tanzania ili iweze kendelea kiuchumi hapa Jijini Tokyo- Japan.
Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Mhe. Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa pamoja na maafisa kutoka Benki ya Dunia wakiendelea na majadiliano juu ya kuangalia uwezekano wa kuisaidia Tanzania ili iweze kendelea kiuchumi hapa Jijini Tokyo- Japan.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia  kwa Bara la Afrika, Bw. Makhtar Diop,akiwa ameambatana na  Maafisa  Waandamizi kutoka Benki ya Dunia wakati wa mazungumzo na Waziri wa Fedha Mhe. William  Mgimwa ambaye yuko na ujumbe wake kutka Tanzania pamoja na Balozi wa  Tanzania nchini Japan Bi. Salome Sijaona  katika kikao cha pamoja cha ambacho Mheshimiwa Waziri alikutana na Kiongozi huyo kwa madhumuni yakutoa mapendekezo ya maeneo ambayo Tanzania tukisaidiwa tutasonga mbele kiuchumi.
Kushoto kwa Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu ni Maafisa kwa Benki ya Dunia wakifuatilia kwa makini kuhusu mkutano huo wakiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania hapa Jijini Tokyo – Japan.Picha Zote na Habari na ingiahedi mduma-Wizara ya Fedha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...