Mshindi wa Top Model Redd's Miss Tanzania 2012,Magdalena Roy (katikati
anaepungia mkono) akiwa na washiriki wenzake alioingia nao hatua ya tano
bora katika shindano
lililomalizika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa hoteli ya Naura
Springs,Jijini Arusha.
MISS Dar City
Center ambaye pia alishika nafasi ya pili katika shindano la Redd’s Miss ilala,
Magdalena Roy amefanikiwa kuingia 15 Bora ya Redd’s Miss Tanzania baada ya juzi
usiku kufanikiwa kutwaa taji la Top Model.
Magdalena
anakuwa mshindi wa pili kuingia katika hatua hiyo, akiungana na Miss Mbulu,
Lucye Stephano ambaye wiki iliyopita alitwaa taji la Miss Photogenic.
Katika shindano
la Top Model lililofanyika kwenye hoteli ya Naura Spring, mjini hapa lilikuwa
na upinzani mkali kutoka kwa washiriki wote wa Redd’s Miss Tanzania.
Mbali na
Magdalena warembo wengine waliofanikiwa kuingia katika tano bora walikuwa ni
Mary Chizi (Ilala), Irene Veda (Lindi), Belinda Mbogo (Dodoma) na Sina
Revocatus (Elimu ya Juu).
Akizungumza na
gazeti hili mjini hapa jana, Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania, Haidan
Ricco alisema warembo hao jana waliondoka kuelekea Tanga kwa ajili ya kutembelea
mapango ya Amboni, kabla ya kurejea Dar es Salaam.
Warembo wapatao
30 wanawania taji la Redd’s Miss Tanzania, ambalo kwa sasa linadhaminiwa na
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.
No comments:
Post a Comment