WAZIRI wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kuwa Tanzania itaendelea
kutafuta msuluhishi wa mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania
kuhusu ziwa Nyasa iwapo nchi hiyo haitaweza kuja kwenye meza ya
mazungumzo juu ya suala hilo kwa kuchukua hatua mbalimbali.
Mazungumzo ya mgogoro huo ambayo
yangetarajiwa kuanzia Oktoba 7 hadi 10, mwaka huu, kinachotarajiwa
kufanyika jijini Dares Salaam.
Aidha Waziri Membe alitoa
pendekezo kwa serikali ya Malawi kwa kuiomba kuwa ikubali timu mbili
zilizokuwa katika mazungumzo hayo zikaendelea kukutana ili kuweza
kupendekeza msuluhishi wa tatizo hilo kwa pamoja.
Kauli hiyo ilitolewa leo na
Waziri huyo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam mara baada ya ziara kurejea nchini hapa kutoka Canada alipokuwa
akihudhuria mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa usiku wa kuamkia leo
kuhusu hatua ya serikali ya Malawi kuandika barua mbili kwa
serikali ya Tanzania mwishoni mwa mwezi uliopita.
Ambapo alisema wamesitushwa na uamuzi huo ,kabla ya kujibu barua hizo.
“Ikiwa Malawi hawatakuja katika
meza ya mazungumzo tutaendelea kutafuta msuluhishi juu ya tatizo hili.
Tumeamua kulimaliza suala hili chini ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Nne
ya Rais Jakaya Kikwete kwa kutumia timu za wataalamu tatu, ambazo ni
wakumbukumbu ambao wataishia kuchukuia kumbukumbu za maisha ya ziwa hili
kabla na baada ya mwaka 1890 nchini Uingereza, pia kukupitia nyaraka
mbalimbali itakazozitumia ”alisema . Waziri Membe.
No comments:
Post a Comment