Waziri wa fedha Dk. William Mgimwa akiongea wakati
wa uzinduzi wa kutumia huduma ya Faraja Bima kupitia M-pesa kwa kushirikiana
na Heritage Insurance, uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene
Meza akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi
wa huduma ya Faraja Bima itakayopatika kupitia M-pesa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Heritage Insurance Bw.Paul
Lewis akisema machache wakati wa uzinduzi huo.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia
Mtingwa kushoto akimsikiliza jambo Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Bw.Matina
Nkurlu, watatu toka kushoto wakati wa uzinduzi wa kutumia huduma ya
Faraja Bima kupitia M-pesa,wapili kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano
ya nje wa Vodacom Tanzania Bw.Salum Mwalim na kulia ni Angela Sompet.
Ofisa Mkuu wa M-Biashara wa Vodacom Jacques
Voogtz (Katikati) akimuonyesha Waziri wa fedha Dk. William Mgimwa namna
ya kujiunga na kutumia huduma ya Faraja Bima kupitia M-pesa baada ya
kuizindua jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom
Tanzania Rene Meza. Kupitia Faraja bima mteja anweza kulipia bima yake
kwa M-pesa.
---
Huduma ya Vodacom ya M-Pesa imezidi kupiga hatua baada ya kuwawezesha
Watanzania kufanya malipo yao ya bima kupitia huduma hiyo.
Hii inafuatia ushirikiano
kati ya Vodacom Tanzania na Heritage Tanzania kuzindua Bima ya
Faraja, ambayo ni Bima ya mazishi ambayo inamuwezesha mlengwa kulipwa
fedha taslim za mazishi kwa muhusika mwenye bima. Bidhaa mbalimbali
ziko katika mpango huo ili kukidhi mahitaji ya wateja na bajeti ya malipo
ya kila mwezi kuanzia shilingi 20000/= fadi 9800/= kwa Mwezi.
Mteja ana chaguo la kuongeza malipo kwa kuongeza
huduma ya vifo vinavyotokana na ajali kulingana na faida na sera zao.
Ongezeko hili la ziada litaongeza kiasi cha faida mara tatu kwa ongezeko
dogo la malipo.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema
wateja wa Vodacom wanaotumia M-Pesa, wataweza kujipatia bima ya bure
kwa mwezi.
“Wateja wetu wote ambao watafanikiwa kutuma pesa
walau mara 10 kwa Mwezi watapata bima ya bure ya kiasi cha Shilingi
laki mbili kwa mwezi unaofuata,” amesema Meza.
Suala la kipekee katika huduma hii ni kwamba hakuna
haja ya kujaza fomu ili kujiunga na bima hii. Mteja atajiunga kwa njia
rahisi kwa kupiga *150*00# na kuchagua kipengele cha bima. Vodacom inahakikisha
kuwa wateja wote wa M-pesa wanaweza kupata huduma hii ili kuwa na amani
ndani ya familia zao.
“Ni muhimu kuthibitisha kuwa taarifa zako
ni sahihi, na kuthibitisha kuwa unaelewa vigezo na masharti. Taarifa
zako zitatumwa moja kwa moja kwenda Heritage Tanzania,” alisema Meza
na kuongeza kuwa, “Unaweza kuchagua aina ya bima ambayo inakidhi mahitaji
na bajeti yako,”
Bima hii ya Faraja pia itawawezesha kila mmoja kubadili au kuongeza
kiwango chake kwa ile yenye faida zaidi kulingana na mahitaji yao na
mabadiliko ya bajeti katika maisha yao.
No comments:
Post a Comment