Pichani Juu na Chini ni Meneja wa MNET Ukanda wa Afrika Mashariki Bi.
Risper Muthamia wakati wa kutangaza rasmi kutolewa kwa Africa Magic
Viewers Choices Awards (AMVCA), ambapo amesema zitawashirikisha Wasanii,
Waandaji na Waandishi wa Filamu kutoka Barani Afrika zitakazofanyika
Lagos nchini Nigeria tarehe 9 Machi 2013.
Bi.
Risper Muthamia amesema kuwa Filamu zote zilizotengenezwa kwa ajili ya
Televisheni na mfululizo wa vipindi vya Luninga (Series) zinaweza
kuwasilishwa kuwania tuzo hizo iwapo zilitengenezwa na kurushwa hewani
au kuonyeshwa hadharani katika kipindi cha kati ya May 1, 2011 hadi
April 30, 2012.
Aidha
amefafanua kuwa Filamu au vipindi vitakavyoshiriki katika tuzo hizo
viwe ni katika lugha ama ya Kiingereza, Hausa (Nigeria), Swahili au
Yoruba na kusisitiza kuwa hakuna Lugha nyingine itakayokubalika.
Ameongeza
kuwa Filamu na Sinema zilizotengenezwa kwa ajili ya Televisheni
zinapaswa kuwa na urefu wa kati ya Dakika 60 mpaka 90 wakati Mfululizo
wa vipindi vya Luninga (Series) ni kwa muda wa dakika 30 mpaka 60.
Wasanii wamekumbushwa kuwa ili kuweza kushiriki katika tuzo hizo
wanapaswa kuwasilisha nakala 6 za DVD za filamu zao.
Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akizungumza
katika semina fupi ya wadau wa tasnia ya Filamu nchini pamoja na
waandishi wa habari na kusisitiza kuwa wasanii watakaopelekea kazi zao
wahakikishe kuwa sio za kuiga na zina hati halali ya kusajiliwa na
COSOTA.
Msanii wa filamu nchini almaarufu kama Mtitu akitoa maoni yake
kuhusiana na tuzo AMVCA zilizoanishwa na Africa Magic kwa kushirikiana
na Multichoice kwa ajili ya kutambua mchango wa wasanii wa bara la
Afrika kwa lengo la kukuza sekta ya filamu Kimataifa.
Wasanii wa filamu wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka Aliyekuwa
msanii maarufu wa filamu Tanzania na Afrika kwa Ujumla aliyefariki dunia
ghafla Marehemu Steven Kanumba.
Msanii wa filamu Cloud naye akichangia mawazo yake wakati wa semina hiyo.
Rais
wa Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba
akiwasisitiza wasanii na watengenezaji wa filamu kuhakikisha zinakuwa na
maudhui ya Kiafrika na ubora unaokubalika.
Bw.
Mwakifamba amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kupenda filamu za
nyumbani na kushiriki katika kuzipigia kura pindi zinapokuwa katika
mashindano ya aina mbalimbali kama itakavyokuwa katika Africa Magic
Viewers Choice Awards (AMVCA).
Meneja
wa MNET Ukanda wa Afrika Mashariki Bi. Risper Muthamia akielezea kuwa
taarifa zaidi kuhusiana na tuzo hizo zinapatikana katika tovuti ya
Africa Magic ambayo ni www.africamagic.tv
na kuwa kiingilio cha kushiriki katika tuzo hizo ni bure na mwisho wa
kuwasilisha fomu za ushiriki ni Oktoba 31, 2012. Kulia ni Meneja Masoko
wa Multichoice Tanzania Furaha Samalu.
Baadhi ya wasanii wa filamu nchini waliohudhu8ria semina fupi
iliyohusiana na Africa Magic Viewers Choice Awards (AMVCA). Kutoka
kushoto ni Msanii Sajuki akiwa amembatana na mkewe na msanii nguli Dkt.
Cheni.
Mchekeshaji na Msanii wa Filamu Steven Nyerere akitoa maoni yake kuhusiana na tuzo hizo.
Meneja
Masoko wa Mutichoice Tannzania Bi. Furaha Samalu sambamba na Meneja
Uhusiano wa kampuni hiyo Barbara Kambogi (wa kwanza kulia).
Yusuf Mlela na msanii mwenzake.
Msanii nguli katika sanaa ya maigizo na filamu hapa nchini almaarufu kama Bi. Mwenda.
Charles Baba naye alikuwepo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Steps Entertainment Bw. Jai (wa pili kushoto) ambao
ni wasambazaji wa filamu nchini akizungumza na maafisa wa kampuni ya
Multichoice.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Bi. Furaha Samalu akibadilishana mawazo na msanii wa Filamu nchini maarufu kama Cloud.
Meneja
Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akiteta jambo na mmoja
wa washiriki wa semina hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam kwa
lengo la kufafanua vigezo vitakavyotumika wakati Africa Magic Viewers
Awards (AMVCA) zinazotarajiwa kufanyika March 9, 2013 Lagos Nigeria.
No comments:
Post a Comment