Habari marafiki, Katika kuelekea siku yangu ya kuzaliwa, yaani October 21, natarajia kufanya yafuatayo.
(1) October 6,nitatembelea moja ya kituo cha kulelea watoto na kuwafariji.
(2) October 7,nitatembelea kambi ya wazee huko Kigamboni na kuwafariji
(3) Otober 13,nitapata
wasaha wa kukaa na watoto wa mtaani wa maeneo mbalimbali waliopo
katikati ya jiji, hii ikiwemo kuwa nao kwa muda wa siku nzima, ikiwemo
maeneo ya Posta,Kariakoo, gerezani,Jangwani na ferri (Hii ni kwa maeneo
yote wanapopatikana waoto hawa.
(4) October 14,
nitakuwa kwenye fukwe za Kigamboni, na marafiki ambapo pia
watakaojumuika siku hiyo watapata kufundishwa namna ya kuogelea kwenye
maji, sambamba na kujiokoa endapo itatokea matatizo.
(5) October October
20,nitatembelea Ocean Road kwenye wodi ya watoto na baadae nitaelekea
Muhimbili kwenye wodi ya watoto na wamama wamama.
…October 21 nitaelekea kanisani na baada ya hapo ni kufurahia kwa pamoja na marafiki./
Ukiwa miongoni mwa #TEAM ANDREW CHALE#
unakaribishwa sana usisite, kwani Andrew Chale, katika maisha yake hapa
duniani anakutegemea wewe na ameishi miaka yote tokea saa 12,jioni,
October 21,1985, alipozaliwa pale Muhimbili Hospital, mpaka leo hii
amekuwa na kufikia hapa ameishi na wewe.
Kwa pamoja, Andrew Chale ambaye awali aliishi katika maisha ya taabu
ikiwemo ya watoto wa Mtaani, na baadae kuachana na maisha hayo (Street
children-3yrs) na baadae kuja kuishi na watu baki (2yrs) na maisha ya
kujitegemea (7yrs) mpaka sasa muda huu.
Hakika kwa neema zake Muumba sina la kumrudishia zaidi ni asante,
kwani licha ya kuwa na shida na taabu kila kukicha najikuta maisha yangu
yanaongezeka mbali ya kutokuwa na kazi ambayo nalipwa mshahara, lakini
nakula, kunywa,nalala,natembea nacheka na hakika wapo watu hapo hapo
ambao wanalipwa mshahara na malupulupu hawaishi kwa raha wanaomba ni
bora wafe…kwa mimi nasema ASANTE MUUMBA.
Ili kufanikisha hili ukiwa umeguswa na unahitaji kuungana name kwenye
kushiriki ukiungana na na #Andrew Chale team#, unaweza kuwasiliana ama
kuwakilisha mchango wako kupitia namba kwa MP PESA ama TIGO PESA- 0719076376 ama 0767076376.
Pia kama utakuwa na vitu ikiwemo nguo ama vyombo ambavyo huvitumii
unaweza wasiliana nami ilikuweza kuvikusanya na kuwafikishia watoto na
watu wasio jiweza.
UNAKARIBISHWA SANA.
No comments:
Post a Comment