Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 5, 2012

NYILAWILA ATOA SABABU ZA KUCHAPWA NA CHEKA PTA


 Na Elizabeth John

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Karama Nyilawila (pichani kushoto) amesema kushinda kwa Francis cheka katika pambano lao si kwamba aliishiwa punzi bali ni kutokana na rafu alizokuwa akifanyiwa na Cheka.

Nyilawila alipigwa kwa KO raundi ya sita na Cheka katika pambano la kuwania ubingwa wa mabara (UBO) uzito wa kg 75 lililofanika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa PTA sabasaba Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Nyilawila alisema faulu alizokuwa akifanyiwa na Cheka ndizo zilizomfanya asalimu amri na kukubali yaishe na kwamba si kweli aliishiwa nguvu za kuendelea kupambana na mpinzani wake.

Kwa upande wake Cheka alisema siri ya yeye kushinda mapambano anayoandaliwa ni kutokana na kufanya sana mazoezi hali inayomjengea kujiamini akiwa ulingoni.

Pia alisema kumpiga Nyilawila kutamaliza minong'ono ya watu waliokuwa wakisema mengi juu yake siku za hivi karibuni.



Cheka ambaye pia ameitaka Serikali na wadau wa michezo kuwekeza udhamini katika mchezo huo ni pambano lake la pili kupigana na Nyilawila.

Katika pambano la awali kati yake na Nyilawila lilifanyika mjini Morogoro na cheka kushinda kwa pointi ambapo hili la marudiano lilikuwa ni la kumaliza ubishi kutokana na baadhi ya watu kudai waamuzi kumpendelea Cheka.

Hata hivyo Cheka mpaka sasa hakuna bondia ambaye aliweza kumtwanga kwa pointi ama KO ambapo tayari ameshamtwanga Rashid Matumla, Mada Maugo, Japhet Kaseba pamoja na mabondia wengine aliokutana nao siku za nyuma.

Bondia huyo kwa sasa amejipanga kujiandaa kwa mapambano atakayokutanishwa na mabondia kutoka nje ya nchi kutokana na kuwamaliza mabondia wa hapa nyumbani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...