Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 5, 2012

SHETTA ANAJIPANGA KUTOKA NA JD


 
Na Elizabeth John

BAADA ya kufanya vizuri katika ngoma yake ya ‘Nidanganye,’ aliyomshirikisha nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum,’ Nurdin Bilal ‘Shetta’amesema kwa sasa ameamua kumshirikisha mwanadada nyota Judith Wambura ‘Lady Jay Dee.’


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Shetta alisema bado hawajapata jina kamili la wimbo huo, ingawa yeye amependekeza uitwe ‘Bonge la Bwana’ kulingana na maneno yaliyotumika ndani ya wimbo, kwamba yataendana na jina hilo.
 

Shetta alisema, ameamua kufanya kazi hiyo na Jay Dee ili kuendelea kuvuta mashabiki katika kazi zake, kutokana na kumkubali mwanadada huyo nguli wa muziki wa kizazi kipya Tanzania, kwani ana imani ngoma hiyo itakuwa nzuri kutokana na sauti yake pamoja na uwezo wake wa kuimba.
 
 
 

“Baada ya ngoma yangu ya ‘Nidanganye’ kufanya vizuri, kwa sasa nimeamua kutoka na mwanadada Jide, naamini uwepo wake katika ngoma hiyo itafanya vizuri, hivyo mashabiki wangu naomba wakae mkao wa kula kuipokea kazi hii,” alisema Shetta.


Mbali na Nidanganye, Shetta alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Maumivu ya Mapenzi’ alichomshirikisha Belle 9, kilichofanya vizuri na kumtambulisha katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...